Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Azimio la Durban na Mpango wa Utekelezaji (DDPA) ni nini?

Watu wa asili kutoka Amazon
PAHO/WHO/Karen González Abril
Watu wa asili kutoka Amazon

Azimio la Durban na Mpango wa Utekelezaji (DDPA) ni nini?

Amani na Usalama

Azimio la Durban Iilipitishwa kwa kauli moja katika mkutano wa dunia wa mwaka 2001 dhidi ya Ubaguzi wa rangi (WCAR) uliofanyika huko Durban, Afrika Kusini.

Azimio hilo DDPA ni hati kamili ya utekelezaji, inayolenga hatua madhubuti za kupambana na ubaguzi wa rangi, ubaguzi mwingine, chuki dhidi ya wageni na masuala mengine ya kutovumiliana.  

Ni ya jumla katika maono yake, na inashughulikia maswala mbalimbali, na ina mapendekezo ya kufikika mbali na hatua za vitendo. 
Dhamira ya azimio hilo. 

Azimio la Durban (DDPA) linajumuisha msisitizo wa kujitolea kwa uthabiti kwa jamii ya kimataifa katika kukabiliana na ubaguzi wa rangi, ubaguzi mwingine, chuki dhidi ya wageni na na hali ya kutouvumiliana katika nagazi zote kuanzia ya kitaifa, kikanda na kimataifa.  

Pia linahimiza kutambua kwamba hakuna nchi inayoweza kudai kuwa haina ubaguzi wa rangi, na nio dhahiri kwamba ubaguzi wa rangi ni suala linalotia hofu ulimwengu wote, na kupambana nao inapaswa kuwa ni juhudi ya za dunia nzima kwani ni mafanikio muhimu.  

Ingawa DDPA sio azimio linalofunga kisheria, lina thamani kubwa ya kimaadili na hutumika kama msingi wa juhudi za uteteziwa haki duniani. 

COVID-19 imeonyesha dhahiri kuenea kwa ubaguzi wa rangi
Unsplash/Thomas de Luze
COVID-19 imeonyesha dhahiri kuenea kwa ubaguzi wa rangi

 Masuala ya kuzingatia kuhusu azimio la Durban (DDPA) 

  1. • DDPA inasisitiza tena kanuni za usawa na kutokuwa na ubaguzi kama haki za msingi za binadamu, na hivyo linahimiza kuwabadili waathirika wa ubaguzi kuwa wamiliki wa haki na mataifa kuwa wahusika wa kufanya hivyo. 
  2. • Kukabidhi jukumu la msingi la kupambana na ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa aina zingine, chuki dhidi ya wageni na kutovumiliana kwa mataifa, DDPA pia inahitaji ushiriki wa dhati wa mashirika ya kimataifa na yasiyo ya kiserikali, vyama vya siasa, taasisi za kitaifa za haki za binadamu, sekta binafsi, vyombo vya habari na asasi za kiraia na jamii kwa ujumla. 
  3. • DDPA inataka dunia nzima kuridhia mkataba wa kimataifa unaohusu kutokomeza aina zote za ubaguzi wa rangi na utekelezaji wake mzuri kutoka pande zote na serikali zote kwenye mkataba huo. 
  4. • DDPA inachukua mwelekeo unaowalenga waathirika wa changamoto za ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa aina zingine, chuki dhidi ya wageni na hali za kutovumiliana. Mapendekezo maalum yameundwa kupambana na ubaguzi dhidi ya Waafrika na watu wa asili ya Kiafrika, Waasia na watu wa asili ya Kiasia, watu wa jamii za asili, wahamiaji, wakimbizi, makundi ya wachache, makundi ya Waroma na vikundi vingine. 
  5. • DDPA inatambua kuwa waathirika mara nyingi wanakabiliwa na aina nyingi za ubaguzi unaozingatia jinsia, lugha, dini, maoni ya kisiasa au maoni mengine, asili ya kijamii, mali, kuzaliwa au hadhi nyingine.  
  6. Inadhihirisha mwelekeo wa kijinsia wa ubaguzi wa rangi na ina jukumu kubwa kwa wanawake katika mipango ya maendeleo ya kupambana na ubaguzi wa rangi na kutovumiliana.  
Mtaalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa dhidi ya masuala ya ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni , ubaguzi na hali zingine za kutovumiliana  profesa Tendayi Achiume
UN Photo/Manuel Elías
Mtaalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa dhidi ya masuala ya ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni , ubaguzi na hali zingine za kutovumiliana profesa Tendayi Achiume

 Hatua za azimio kuzuia ubaguzi wa rangi

  1. •   DDPA inasisitiza umuhimu wa hatua za kuzuia na za pamoja, haswa katika uwanja wa elimu na kukuza uelewa, na inatoa wito wa kuimarishwa kwa elimu ya haki za binadamu. 
  2. •   DDPA inataka mipango kamili ya kitaifa ya kutokomeza ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa aina zingine, chuki dhidi ya wageni na hali ya kutovumiliana. Inahitaji kuimarishwa kwa taasisi za kitaifa na imeandaa mapendekezo madhubuti katika maeneo ya sheria za kitaifa na usimamizi wa haki. 
  3. •   DDPA inaelezea hatua za kushughulikia ubaguzi katika nyanja za ajira, afya, polisi, na elimu. Pia inatoa wito kwa mataifa kupitisha sera na programu za kukabiliana na uchochezi wa chuki za rangi katika vyombo vya habari, pamoja na wavuti. Inahitaji ukusanyaji wa takwimu zilizogawanywa, pamoja na utafiti wa ziada, kama msingi wa kuchukua hatua zilizolengwa. 
  4. •   DDPA inayachagiza mataifa kuchukua hatua chanya ili kutoa fursa sawa kwa waathirika wa ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa aina zingine, chuki dhidi ya wageni na wa hali ya kutovumiliana katika nyanja za maamuzi ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni. 
  5. •   DDPA inazitaka serikali kutoa suluhisho bora, kubadili mwelekeo, kurekebisha na kuchukua hatua za kulipa fidia kwa waathiriwa na kuhakikisha kuwa wanapata msaada wa kisheria ili waweze kufuata hatua hizo. Pia inapendekeza kuundwa kwa mashirika ya kitaifa yenye uwezo wa kuchunguza vya kutosha madai ya ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa aina zingine, chuki dhidi ya wageni au hali zinazohusiana na kutovumiliana. 
  6.  •   DDPA inakubali kuwa utumwa na biashara ya watumwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu, na ingelipaswa kuwa hivyo kila wakati. Inaelezea majuto juu ya ukweli kwamba biashara ya watumwa na ukoloni ulichangia kudumu kwa pengo la usawa la kiuchumi na kijamii. Linakaribisha juhudu za mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO ujulikanao kama “mradi wa njia ya utumwa”. 

  Azimio la Durban kuhusu mustakbali wa Palestina 

  1.  • Kuhusu Mashariki ya Kati, DDPA inaelezea wasiwasi wake juu ya madhila yanayowakabili watu wa Palestina chini ya uvamizi wa kigeni na inatambua haki isiyoweza kutengwa ya watu wa Palestina ya kujitawala na haki ya kuwa na serikali huru. Inatambua pia haki ya usalama kwa nchi zote katika eneo hilo, pamoja na Israeli, na inatoa wito kwa serikali zote kuunga mkono mchakato wa amani na kuufikia ukomo wa madhila hayo. 
  2. •  DDPA inakumbusha kwamba mauaji ya maangamizi makuu ya Holocaust yasisahaulike kamwe. 
  3. •  Mwisho, programu ya utendaji ya azimio la Durban inaelezea mikakati kadhaa ya kufikia usawa kamili na ufanisi kupitia ushirikiano wa kimataifa. Mikakati inajumuisha mfumo madhubuti wa sheria za kimataifa, ushirikiano wa kikanda na wa kimataifa ulioimarishwa, jukumu muhimu kwa ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, na ushiriki wa wadau mbalimbali, pikiwemo asasi za kiraia, mashirika yasiyo ya kiserikali na vijana katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa aina zingine, chuki dhidi ya wageni na na masuala yanayohusiana na hali ya kutovumiliana .