Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naibu Katibu Mkuu Amina J. Mohammed afanya ziara nchini Tanzania

Naibu Katibu Mkuu Amina J. Mohammed amefanya ziara nchini Tanzania na amefanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan, katika Ikulu ya Chamwino, Mkoani Dodoma.
Ikulu Tanzania
Naibu Katibu Mkuu Amina J. Mohammed amefanya ziara nchini Tanzania na amefanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan, katika Ikulu ya Chamwino, Mkoani Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Amina J. Mohammed afanya ziara nchini Tanzania

Masuala ya UM

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed, amefanya ziara maalum ya siku mbili nchini Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 

Katika ziara yake leo   tarehe 11 Septemba, 2021amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan, katika Ikulu ya Chamwino, Mkoani Dodoma.

Katika mazungumzo hayo Bi.Mohammed amewasilisha salamu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres na kumpongeza Rais Samia kwa kushika nafasi ya Urais na kumtakia heri katika majukumu yake.

Amemuhakikishia Rais Samia kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kumuunga mkono katika jitihada zake mbalimbali za kuiletea maendeleo Tanzania, ikiwemo kufikia malengo ya maendeleo Endelevu (SDGs).

 Aidha, amempongeza Mhe. Rais Samia kwa jitihada anazochukua dhidi ya janga la COVID-19 ambapo amesema Umoja wa Mataifa unaendelea kuhakikisha kuwepo na usawa wa upatikanaji wa chanjo na wanaendelea na majadiliano na taasisi za Kifedha kuona ni jinsi gani zinasadia nchi zinazoendelea kukabiliana na ugonjwa huo.

 Vilevile, ameahidi kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita za kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama.

Kwa upande wake Rais Samia amempongeza Bi Amina J. Mohammed kwa kuteuliwa tena kushika nafasi hiyo ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kumhakikishia ushirikiano zaidi kwa kuwa Umoja wa Mataifa kupitia taassisi zake mbalimbali ni mbia wa maendeleo nchini.

 Rais Samia amemueleza kuwa serikali yake inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ambapo katika kipindi cha miezi mitatu idadi ya wawekezaji imeongezeka.

NB: Taarifa ya Ikulu Tanzania