Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mustakabali wa UN: Ni wakati wa kutafakari kwa mapana zaidi, anahimiza Guterres 

Wanafunzi wakiwa shuleni huko Hanoi, nchini Viet Nam.
UN Photo/Mark Garten)
Wanafunzi wakiwa shuleni huko Hanoi, nchini Viet Nam.

Mustakabali wa UN: Ni wakati wa kutafakari kwa mapana zaidi, anahimiza Guterres 

Masuala ya UM

Ripoti  mpya ya kihistoria ya “Ajenda Yetu ya Pamoja” imetolewa leo Ijumaa Septemba 10, 2021 na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ikielezea maono yake ya siku zijazo za ushirikiano wa kimataifa. 

Wakati wa maadhimisho ya miaka 75 ya Umoja wa Mataifa mwaka jana, kulizuka majadiliano makubwa ya ndani kuhusu mustakabali shirika hilo kubwa zaidi la kimataifa duniani , na mwelekeo mpya mbali na makubaliano ya wakati wa vita mbili kubwa za dunia katika siku za mwanzo za uwepo wa shirika hilo. 

Na tafakari hizi zimesababisha “Ajenda Yetu ya Pamoja” imesema ripoti mpya ya kihistoria iliyotolewa leo Ijumaa Septemba 10, 2021 na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ikielezea maono yake ya siku zijazo za ushirikiano wa kimataifa. 

Guterres amezindua ripoti hiyo katika mkutano wa Baraza Kuu unaofanyika mjini New York Marekani leo akielezea hali ya dunia kuwa chini ya shinikizo kubwa, na kuonya kwamba ulimwengu unahatarisha hali ya maisha ya baadaye ya kughubikwa na kukosekana kwa utulivu na machafuko yatokanayo na mabadiliko ya tabnianchi. 

"Kuanzia mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi hadi vita vyetu vya kujiua kwa kuharibu mazingira na kutoweka kwa bioanuwai, mwitikio wetu wa hatua za kimataifa ni kidogo sana, na umechelewa sana", amesema Katibu Mkuu na kuongeza kuwa "Ukosefu wa usawa ambao haujadhibitiwa unadhoofisha mshikamano wa kijamii, na kuunda udhaifu unaotuathiri sisi sote. Teknolojia inasonga mbele kwa kasi bila mbinu za kutulinda kutokana na athari zake zisizotarajiwa. " 

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameendelea kuelezea mashauriano mengi ambayo yameleta maendeleo na zoezi la kusikiliza maoni ambalo lilipelekea Umoja wa Mataifa kuhitimisha kuwa kuimarika kwa mshikamano wa kimataifa kunaonekana kama njia ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia kuvunjika au kufanikiwa.
 

Kimbunga Matthew kilisababisha maporomoko ya ardhi huko Port-au-Prince nchini Haiti
UN Photo/Igor Rugwiza
Kimbunga Matthew kilisababisha maporomoko ya ardhi huko Port-au-Prince nchini Haiti

Ripoti inasema kuna hatima mbili tofauti: mosi ya kuvunjika na kuleta shida ya kudumu, na pili ni ile ya kuwa na mafanikio, kwa siku za mustakabali bora na salama. 

Hali ya siku ya mwisho inaelezea ulimwengu ambao COVID-19 inabadilika bila kikomo, kwa sababu nchi tajiri huhifadhi chanjo, na mifumo ya afya imezidiwa. 

Katika mustakbali huo, sayari inakuwa isiyoweza kukaliwa na watu kutokana na kuongezeka kwa joto na hali mbaya ya hewa, huku viumbe milioni viko kwenye hatihati ya kutoweka. 

Hii inaambatanishwa na mmomonyoko wa haki za binadamu unaoendelea, upotezaji mkubwa wa ajira na mapato, na kuongezeka kwa maandamano na machafuko, ambayo yanakabiliwa na ukandamizaji mkali. 

Au, ripoti inasema “tunaweza kwenda kwa njia nyingine, tukishiriki chanjo kwa usawa, na kusababisha ahueni endelevu ambayo uchumi wa ulimwengu unahitaji ili hurejeshwa upya kuwa endelevu zaidi, wenye mnepo na unaojumuisha wote.” 

Kwa kukomesha hewa ukaa, ongezeko la joto ulimwenguni lingekuwa dogo, na nchi zilizoathiriwa sana na mabadiliko ya tabianchi zingeungwa mkono, na mifumo ya ikolojia itahifadhiwa kwa ajili ya vizazi vijavyo, imesema ripoti. 

Mtazamo huu ungeweza kutangaza enzi mpya kwa ushirikiano wa kimataifa ambapo nchi zinafanya kazi pamoja kutatua shida za ulimwengu; mfumo wa kimataifa unafanya kazi haraka kulinda kila mtu katika dharura; na Umoja wa Mataifa unatambuliwa ulimwenguni kama jukwaa la kuaminika kwa ajili ya ushirikiano

Usambazaji wa chakula wakati wa janga la coronavirus huko Bangladesh. (faili)
UNDP/Fahad Kaizer
Usambazaji wa chakula wakati wa janga la coronavirus huko Bangladesh. (faili)

 

 Mustakbali bora: Malengo na suluhisho 

Ili kuhakikisha kuwa tunaishi katika ulimwengu ambao hali ya mafanikio inatawala, ripoti hiyo inafanya imetoa msururu wa mapendekezo muhimu.

Umuhimu wa kulinda vikundi vilivyo hatarini unatambuliwa katika mkakati wa usawa wa kijinsia na kutokumuacha mtu yeyote nyuma, ambao unachagiza kuimarisha ulinzi wa kijamii na kukuza usawa wa kijinsia. 

Pia kuhakikisha uchumi endelevu zaidi duniani kunatambuliwa kama lengo, na msaada kwa watu maskini, na ni mfumo mzuri wa biashara ya kimataifa. 

Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi pia zinatajwa maalum katika ripoti hiyo, na ahadi kwa lengo la kupunguza joto hadi kufikia nyuzi joto 1.5C juu ya viwango vya kabla ya maendeleo ya viwanda, na kukomesha uzalishaji wa hewa ukaa ifikapo mwaka 2050, pia kukomesha ruzuku ya mafuta kisukuku, mabadiliko ya mifumo ya chakula, na kifurushi cha msaada kwa nchi zinazoendelea.

Maswala ya kudumu ya amani na usalama yanashughulikiwa, na ripoti hiyo inataka "ajenda mpya ya amani", ikijumuisha uwekezaji zaidi kwa ujenzi wa amani, msaada kwa kuzuia migogoro ya kikanda, upunguzaji wa hatari za kimkakati kama vile silaha za nyuklia na vita vya mtandao na mazungumzo kwenye anga za juu kuhakikisha kuwa inatumiwa kwa amani nakwa uendelevu. 

Kinachohusishwa na suala la usalama ni ahadi kwa haki ya kimataifa; utekelezaji za haki za binadamu mtandaoni, kama sehemu ya Mkataba wa kimataifa wa masuala ya kidijitali, na kuongeza hatua katika vita dhidi ya ufisadi, kwa lengo la kujenga imani kwa taasisi. 

Walinda amani kutoka kikosi cha Ivory Coast katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka amani Mali, MINUSMA, wanashika doria.
MINUSMA
Walinda amani kutoka kikosi cha Ivory Coast katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka amani Mali, MINUSMA, wanashika doria.


Wakati Umoja wa Mataifa unapoanza muongo mmoja wa utekelezaji -miaka 10 kufanya maendeleo ya kweli kutoa ahadi ya mustakbali endelevu, mzuri wa baadaye na ajenda yam waka 2030 kuna fursa ya kuubadilisha ulimwengu kuwa bora, na umoja wa nchi katikati ya mchakato. 

Walakini, kama "hali ya kuvunjika" inavyoonyesha, kutofaulu kufanya kazi kwa pamoja kuna hatari kubwa, isiyoweza kurekebishwa kwa sayari yetu na hata, maisha yenyewe. 

Katika hotuba yake kwa Baraza Kuu Bwana. Guterres amesisitiza kwamba Ajenda Yetu ya Pamoja inaongozwa na mshikamano, "Kanuni ya kufanya kazi pamoja, kutambua kwamba tumeunganishwa na kila mmoja na kwamba hakuna jamii au nchi, hata ikiwa ina nguvu kiasi gani, inayoweza kutatua changamoto zake peke yake." 


 Muktadha: Ajenda yetu ya Pamoja 


• Ukweli kwamba maadhimisho ya miaka 75 yalikuja wakati wa dharura ya kiafya duniani, inaonyesha umuhimu wa mawazo ya kimataifa: mwaka 2020 uliona kuibuka kwa janga la COVID-19, ambalo lilikuja wakati wa wasiwasi mkubwa wa changamoto ya mabadiliko ya tabianchi, suala lingine la haraka ambalo haliheshimu mipaka ya kitaifa. 
• Mapema mwaka 2020, watu milioni 1.5 walishiriki katika mpango wa Umoja wa Mataifa wa mwaka mzima kusikiliza vipaumbele vya watu, na matarajio ya jinsi ushirikiano wa kimataifa unaweza kuathiri mustakbali wa dunia. 
• Walishiriki matumaini yao na hofu yao, wakitaka Umoja wa Mataifa ulio wazi zaidi, unaojumuisha wote, na kutambua mabadiliko ya hali ya hewa na maswala ya mazingira kama changamoto namba moja ya muda mrefu ulimwenguni. 
• Ajenda yetu ya pamoja iatokana na matokeo ya mpango huo  na maoni kutoka kwa viongozi mbalimbali, vikundi maarufu kama wazee, wanadiplomasia na washirika wengine - wakitoa maoni na suluhisho, maoni ya kuchukua  hatua, na kutazamia miaka 25 ijayo ya Umoja wa Mataifa. 
• Ripoti hiyo inataka maadili ya msingi ya Umoja wa Mataifa yasimamishwe tena, wakati ikikubali kwamba misingi ya Shirika, inahitaji kubadilishwa ili kuakisi ulimwengu wa leo. 
• Ripoti iligundua pia hitaji la dharura la kuchukua hatua: mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi unasababisha mgogoro uliopo kwa maisha yote ya wanadamu, na unaweza kutatuliwa tu ikiwa jamii ya kimataifa itafanya kazi kwa pamoja, kuvuka mipaka, kumaliza kasi ya kuathiri sayari inayosababishwa na shughuli za kibinadamu, na kukabiliana na uharibifu ambao tayari umeshatokea i.