Ninalaani utwaaji wowote wa serikali kwa mtutu wa bunduki - Antonio Guterres 

5 Septemba 2021

Kufuatia taarifa za wanajeshi wa Guinea kumshikilia Rais wa nchi hiyo Bwana Alpha Conde na kutangaza kuipindua serikali, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma ujumbe kupitia katika ukurasa wake wa Twitter akitoa wito wa kuachiliwa kwa Rais Conde.

"Mimi binafsi ninafuatilia kwa karibu sana hali ilivyo nchini Guinea. Ninalaani vikali utwaaji wowote wa serikali kwa nguvu ya bunduki na nataka kuachiliwa mara moja kwa Rais Alpha Conde." Umesema ujumbe wa Guterres. 

Kufuatia video ambayo haijathibitishwa kumwonesha Rais Conde akionekana kuwa chini ya ulinzi wa wanajeshi wanaaonekana kumzonga kwa maneno, duru zinadai kwamba wanajeshi wa nchi hiyo wameipindua serikali ya Guinea ingawa vyombo vingine vya habari vinaeleza kuwa Waziri wa ulinzi wa nchi hiyo amedai kuwa jaribio la wanajeshi kuitwaa serikali ya Alpha Conde limeshindwa.

 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter