Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake; nchini Uganda wachukua hatua mbele baada ya sheria muhimu kupitishwa na bungeni

Msichana anayejishughulisha na kilimo na ufugaji akimwagilia mazao nchini Uganda
©FAO/Luis Tato
Msichana anayejishughulisha na kilimo na ufugaji akimwagilia mazao nchini Uganda

Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake; nchini Uganda wachukua hatua mbele baada ya sheria muhimu kupitishwa na bungeni

Wanawake

Kurekebisha sheria iliyopitwa na wakati ambayo pia ilikuwa baguzi ni hatua muhimu kutokomeza ukatili dhidi ya wanawwake na wasichana shirika la wanaharaki wa haki za wanawake lilihakikisha hatua muhimu imechukuliwa mnamo 2021. 

Baada ya miongo ya utetezi na uanaharakati wanaharakati wa haki za wanawake wana sababu ya kusherelekea mwaka huu nchini Uganda – wamekaribisha kwa shangwe hatua ya bunge la nchi hiyo kupitisha marekebisho ya sheria mbili zilizokuwa zimepitwa na wakati.

Mnamo Machi, kupitishwa kwa marekebisho ya mswada wa urithi ilikuwa ni hatua ya kushughulikia ukuikwaji wa kihistoria wa haki za wanawake na wasichana za umiliki wa mali kwani sheria ilikuwa ikijigemea kwa wanaume au watoto wa kiume wakati wa urithi wa ardhi au umiliki wake. 

Bila uwezekano wa kupata kipato na ardhi ambapo nyumba salama inaweza kujengwa haki za wanawake na wasichana wengi zilikuwa hatarini kukiukwa.  

“Sheria ya zamani na mapengo katika sheria nchni Uganda, umiliki wa mali ulikuwa ni wa kurishishwa kama zawadi na kwa watoto wa kiume na wanaukoo,” aeleza Tina Musuya, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Center for Domestic Violence Prevention (CEDOVIP). 

 

 “Wanawake wengi na wasichana, ambao hawana pesa, wasingeweza kununua ardhi,” aliongeza. 

 

“Mara nyingi wajane walikuwa wakifukuzwa majumbani na wanafamilia. Sheria mpya inashughulikia mianya ifuatayo; watoto (wavulana au wasichana) kwa sasa wanatambuliwa kwa usawa kuwa na haki ya kumiliki mali. Mswada huu utasomga mbele zaidi katika kushughulikia watoto tegemezi na kulind ahaki za wanawake,” asema Musuya. 

 

Siku chache badaye, mnamo Aprili, marekebisho ya mswada wa ajira pia yalipitishwa, ikimaanisha kwamba waajiri kwa sasa wanatakiwa kuweka mikakati kuzuia unyanyasaji wa kingono kazini na kuzuia udhalilishaji au ukatili wowote dhidi ya wafanyakazi.

“Mswada huu unashughulikia pia wafanyakazi wa nyumbani ambao hawalipwi kabisa au kwa wakati mwafaka. Kazi yao kwa sasa inatambuliwa rasmi; wanapaswa kulipwa na kulindwa dhidi ya ukatili kukiwa kuna mikakati ya kuripoti ukatili wowote unapotokea,” aeleza Musuya akiongeza kuwa, “Mswada huu pia unahakikisha ulinzi wa wafanyakazi wote wakiwemo wanawake wengi wanaoajirwa katika biashara ndogondogo sizizo rasmi ambao huwa hatarini kunyanyaswa  kingono na  kunyonywa.” 

Wakishirikiana pamoja wanawake wanaharakati nchini Uganda kwa kipindi cha karibu miongo miwili, wamefanikiwa kushughulikia mapengo ya kisera na sheria vilivyokuwa vinakwamisha usawa wa kijinsia na kukiuka haki za wanawake nchini humo. 

Kwa kutambua umuhimu wa kurekebisha sheria baguzi, UN Women kama sehemu ya kikundi cha EU cha kila mwaka- UN Spotlight Initiative cha kutokomeza ukatli dhidi ya wanawake na wasichana, walianzisha kutafuta rasilimali ili kusaidia CEDOVIP na mashirika mengine ya wanawake katika mwaka wa 2019. 

“CEDOVIP ikiwa ni mratibu wa Muungano wa kushinikiza sheria ya Mizozo ya Nyumbani, ilikuwa ni muhimu sana kwetu kushiriki katika juhudi za kutetea miswada hii,” asema Musuya.  

Musuya anaendelea kueleza kuwa, “Tulishiriki kwenye juhudi za kujadiliana na watunga sera na wadau wengine muhimu. Kiwango cha ukatili dhidi ya wanawake ni jambo pana na ni vyema kukubali kwamba sheria moja tu haitaweza kulishughulikia.” 

Msaada uliotolewa na ‘Spotlight Initiative’ ulisababisha kuwezeshwa kwa watetezi wa haki za binadamu na wanahabari, na kuwezesha mikutano na wabunge na kutoa mafunzo kwa kamati za bunge. 

“Haijawa safari rahisi kuhakikisha marekebisho ya mswada wa urithi,” anasema Mary Harriet Lamunu, Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha wabunge wanawake wa Uganda (Uganda Women Parliamentary Association (UWOPA), katika kipindi cha kupitisha mswada huo. 

 

Mary Lamunu anasema, “nafurahia kupitishwa kwa mswada huu kutokana na juhudi zetu kama watalaamu tukisaidia wabunge kuelewa muktadha wafaidika wa kuwa na sharia nyeti.” 

 

Ikiwa miswada imepitishwa sasa na Bunge, hatua inayofuata ni kuona kwamba yote imetiwa saini na Rais wa Uganda. Utekelezaji wa sheria hizo utaaza punde tu baada ya kutiwa saini na rais. Mradi huu wa Spotlight Initiative utaendelea kuunga mkono harakati za wanawake katika uwezo wa kisheria na kuelimisha umma kuhusu sheria. Pia kuna uwezo wao kuishinikiza serikali kufadhili utekelezaji wake na kutetea mabadiliko ya kitaasisi katika mfumo wa sheria na sekta nyingine mkakati mwafaka wa kuwezesha sheria hiyo kutekelezwa.  

“Kupitishwa kwa miswada hii kulitokana na juhudu kubwa endelevu na ushirikiano,” asema Agripinner Nandhego, Mtalamu wa UN Women Uganda kuhusu ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi. 

“Kazi kubwa ilifanywa na asasi za kiraia, UWOPA, muungano wa dini, na wanaharakati binafsi. Msaada kutoka wabunge wa kiume nao pia ulikuwa muhimu,” anaongeza pia kwamba, “utetezi huu wa pamoja na mafanikio yale ni ishara ya kile tunachoweza kupata katika sera na sharia tukiwa na wanaharakati wanawake.”