Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kudhibiti saratani za utotoni kwa kubaini na matibabu ya mapema:WHO

Mtoto wa miaka miwili na mama yake  akisubiri kuonana na Daktari kwa masuala ya Kansa kwa watoto hospitalini Accra, Ghana
WHO/Ernest Ankomah
Mtoto wa miaka miwili na mama yake akisubiri kuonana na Daktari kwa masuala ya Kansa kwa watoto hospitalini Accra, Ghana

Kudhibiti saratani za utotoni kwa kubaini na matibabu ya mapema:WHO

Afya

Wakati wa moja ya safari za mara kwa mara za Naomi Otua kumtembelea mjukuu wake James katika mji wa Assin Fosu kati kati mwa Ghana, aligundua kuwa kulikuwa na tatizo kubwa sana.

Aliona macho ya mjukuu wake wa umri wa miaka 10 yalikuwa yamegeuka rangi na kuwa ya njano na pia alikuwa amepungua sana uzito. 

Kutokana na hofu aliyokuwa nayo alimpeleka Otua kwenye hospitali ya serikali  ya Suhum.

Kisha James akatumwa kwenda hosptali iliyo eneo la Koforidua Mashariki mwa nchi hiyo ambako alikaa kwa wiki tatu. 

Lakini hali yake ilizidi kudhoofika na kisha ikambidi kupelekwa kwenye hospistali nyingine ya Korle-Bu iliyo kwenye mji mkuu wa Ghana Accra ambapo iligunduliwa kuwa alikuwa anagua saratani ya damu.

Mgonjwa wa saratani akijiandaa kwa tiba ya mionzi
IAEA/Dean Calma
Mgonjwa wa saratani akijiandaa kwa tiba ya mionzi

Zaidi ya watoto 400,00 wanaugua saratani kila mwaka

James ni mmoja wa takriban watoto 400,000 wanaogundiliwa kuugua saratani kila mwaka kote duniani.

Nchini Ghana takiban watoto 1,200 walio chini ya umri wa miaka 15 wanakadiriwa kuugua saratani kila mwaka.

Muda mfupi baada ya kuwasili Korle-Bu na kugundukiwa kuugua saratani, James alianza matibabu ambayo yameendelea kwa miezi mitatu sasa. “Hali yake imeimarika sana,” anasema nyanya yake Otua baada ya karibu miezi sita migumu ya kuzuru hospitali tofauti.

Kwa mujibu wa Prof Lorna Awo Renner mkuu wa kitengo kinachoshughulikia magonjwa ya watoto hospitali ya Korle-Bu, asilimia 80 ya saratani za  watoto hutibiwa, lakini hii hutegemea na ugonjwa huo kugunduliwa mapema

Licha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya watoto walio ma saratani huishi kwenye nchini zinazoendelea kama Ghana, ni asilimia 20 hadi 30  kati ya hao ndio hupata matibabu kama hayo na hii mara nyingi hutokana na gharama kubwa ambazo wengi hawawezi kumudu.

Gharama za matibabu

Nchini Ghana ambapo matibabu ya maradhi ya saratani hayagharamiwi na bima ya afya ya serikali, gharama ya kutibu saratani ya utotoni ni karibu dola 1,000, Kwa kutibu saratani ya damu gharama inaweza kufika hadi dola 7,000 kwa hadi kipindi cha miaka mitatu. Gharama hii ni kubwa sana kwa watu wengi nchini Ghana kuweza kumudu.

Nchini Ghana karibu asilimia 50 ya wagonjwa walikuwa wakiachia matibabu njiani kufuatia ukosefu wa fedha. Lakini idadi hii imeshuka hadi asilimia 15 kutokana na misaada kutoka kwa watu na mashirika.

Mwaka 2018 shirika la afya duniani WHO lilitangaza mpango mpya wa dunia nzima kugharamia saratani za utotoni ambapo Ghana ilikuwa moja ya nchini zilizochaguliwa kupata msaada huo.

 “Kwa kushirikiana kwa karibu na serikali ya Ghana, tumesadia kuhakikisha uwepo wa mpango wa kiwango cha juu unaohusu saratani ya utotoni ukiwa na lengo la kuhakikisha asilimia 60 ya watoto wanaishi ifikapo mwaka 2030,”  amesema Dr Francis Kasolo, mjumbe wa WHO nchini Ghana.

Licha ya kuwepo uhaba wa vifaa na wahudumu wa afya katika hospitali ya Korle-Buambapo wamepata misaada ya kiufundi kutoka WHO, kujaribu na kuhakisha kuwa watoto wagonjwa wamepata huduma ya hali ya juu inayostahili.

“Kuwaona watoto wakitabasamu na kucheza hutuletea furaha sana. Ni ishara kuwa wanapata nafuu kila siku na kuwa tiba inafanikiwa,” anasema Leticia Amengor muuguzi katika kitengo hicho cha saratani.

Kwa Prof Renner, kuwaruhusu watoto kurudi nyumbani mara inapobainika kuwa wamepona ni jambo la huridhisha. Ana imani kuwa hivi karibuni James ataushinda ugonjwa na kuruhusiwa. “Watoto hawa bado wanaweza kuishi maisha ya kawaida,” anasema, “nimeshuhudia haya yakitokea mara kwa mara.”

TAGS: UNICEF, watoto, saratani, Ghana