Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

TANBAT4 yakarabati daraja kuwaondolea adha wananchi CAR

Ukarabati wa daraja katika jimbo la Amadagaza-Mambere Kadei na TANBAT4 chini ya MINUSCA.
MINUSCA/Noella Nyaisanga
Ukarabati wa daraja katika jimbo la Amadagaza-Mambere Kadei na TANBAT4 chini ya MINUSCA.

TANBAT4 yakarabati daraja kuwaondolea adha wananchi CAR

Amani na Usalama

Walinda amani kutoka kikosi cha 4 cha Tanzania au TANBAT-4 kinachohudumu nchini Jamhuria ya Afrika ya Kati CAR kimekarabati daraja lililovunjika kwa muda mrefu na kusababisha adha kubwa kwa raia wa jimbo la Amadagaza-Mambere Kadei. Kukamilika kwa ukarabati huo ni faraja kubwa kwa raia wa eneo hilo.

Jukumu kuu la kikosi hicho cha ulinzi wa amani hapa CAR ni ulinzi wa raia, lakini mbali na jukumu hilo TANBAT-4 imekuwa ikijushughulisha na shughuli zingine mbalimbali za kijamii katika jimbo la Amadagaza-Mambere Kadei.

Mathalani hivi karibuni kikosi hicho kimeweza kuwaondolea adha kubwa raia wa eneo hilo ambao walishindwa kusafirisha bidhaa muhimu kwa ajili ya maisha ya kila siku ikiwemo chakula, bidhaa za kiuchumi na mahitaji mengine baada ya daraja kuu walilokuwa wakilityegemea kubomoka.

Ukarabati wa daraja hilo kwa mujibu wa kapteni Frederick Osmond Mchimbi Miongoni mwa walinda amani walioshiriki katika ukarabati ni muhimu sana sio tu kwa kukidhi mahitaji ya msingi ya kila siku kwa raia bali pia kwa shughuli za kiuchumi zinazowaingizia kipato

Ukarabati wa daraja hili liliclochukua miezi kadhaa kukamilika ni sehemu tu ya shughuli nyingi za kusaidia jamii zinazofanywa na kikosi cha TANBAT-4 hapa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati mbali ya jukumu lao kubwa la ulinzi wa raia.