Skip to main content

Mradi wa Fao wa Fish4ACP Kigoma Tanzania kuwakomboa wavuvi 

Samaki waliovuliwa kwenye shamba la samaki la familia kufuatia mfumo wa umwagiliaji unaovuta maji kutoka mto ulio jirani.
UN Photo/Logan Abassi
Samaki waliovuliwa kwenye shamba la samaki la familia kufuatia mfumo wa umwagiliaji unaovuta maji kutoka mto ulio jirani.

Mradi wa Fao wa Fish4ACP Kigoma Tanzania kuwakomboa wavuvi 

Ukuaji wa Kiuchumi

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa mataifa FAO limewaalika waandishi wa habari katika ziara ya siku nne mkoani kigoma nchini Tanzania ili kutembelea miradi yake hususan ya uvuvi Fish4ACP mkoani humo ambayo itakuwa na manufaa makubwa kwa wakazi wa mkoa huo na kwingineko

Matembezi hayo ya siku nne yanafanyika katika maeneo mbalimbali yakiwemo  Katonga na Kibirizi kwa lengo la kuona shughuli zinazofanywa na wavuvi wadogowadogo  katika ziwa Tanganyika  na changamoto zinazowakabili kupitia mradi wa FISH4ACP  wa miaka mitano unaotekelezwa na FAO ambao ulianza  rasmi mwezi Septemba 2020. 

Akizungumza na UN News, afisa mtaalamu mnyororo wa thamani wa Uvivu na ufugaji viumbe Maji, kutoka FAO Tanzania anayesimamia mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma, Hashim Muumin amesema mradi huo unatekelezwa katika Nchi 12 za Afrika ikiwemo Tanzania. 

Afisa huyo amesema lengo la kuanziashwa kwa mradi ni kuboresha Uvuvi wa ziwa Tanganyika kwa kuwapatia  mafunzo bora ya uhifadhi na uchakataji wa mazao ya uvuvi, kuwapa elimu ya uhifadhi wa rasilimali za uvuvi, kuongeza uhakika wa chakula, na kuboresha maisha ya wadau wa mnyororo wa thamani wa uvuvi wa ziwa hilo ambapo kwa sasa hatua iliyofanyika ni ukusanyaji wa  taarifa na kuziandikia report kwa mikoa yote mitatu. 

Hatua itakayofuata ni utekelezaji wa  mikakati ya kufungua fursa zilizokuwepo katika mnyororo wa thamani kwa samaki wa migebuka na dagaa wa ziwa tanganyika. 

Naye afisa uvuvi wa Halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji ,Mariki Mdetele amekiri uwepo wa mradio huo katika Halmashauri yako akisema umekuja wakati muafaka kuwezesha wavuvi wadogo na wafanyabiashara wa samaki na dagaa kuongeza thamani ya bidhaa zao na kuongeza wigo wa masoko. 

Nao baadhi ya wavuvi na wafanya biashara wakazungunzia ujio wa mradio huo na namna utakavyowanufaisha kufanya shughuli zao kuendana na ukuaji wa teknolojia  kuondokana na Uvuvi wa mazoea hatimaye kuvua kisasa. 

Mradi huo wa FISH4ACP unafadhiliwa na Muungano wa Ulaya.