Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikundi vipya vya vijana wenye silaha vyaibuka nchini Sudan Kusini

Watu walioyakimbia makazi yao katika eneo la Equatoria Magharibi Sudan Kusini
UNMISS
Watu walioyakimbia makazi yao katika eneo la Equatoria Magharibi Sudan Kusini

Vikundi vipya vya vijana wenye silaha vyaibuka nchini Sudan Kusini

Amani na Usalama

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS umeeleza kuwa hali ni mbaya kwenye eneo la Tambura katika jimbo la Ikweta Magharibi kutokana na kuongezeka kwa vikundi vya vijana wenye silaha waliotokea katika jamii za Azande na Balanda.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini New York nchini Marekani Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema UNMISS imeimarisha ulinzi wake kwa  wakimbizi wa ndani walioko katika eneo hilo.

UNMISS imewaondoa wafanyikazi wa kusaidia masuala ya kibinadamu katika eneo hilo ambao walikuwa wamekimbilia kituo chao cha muda cha kufanya kazi kutokana na machafuko”.

Dujarric ameongeza kuwa ujumbe unatuma wa wanajeshi wengine kuimarisha kambi hiyo baada ya kuwasili kwa wakimbizi wapya wa ndani waliofika hapo kutafuta makazi na ulinzi wakikimbia machafuko katika vijiji vyao.