Skip to main content

Tunatakiwa kusherekea utajiri wa dini zetu na sio chuki: Guterres

Msichana mdogo anashikilia ishara inayosema Zo Kwe Zo, wito wa kitaifa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati,  ikimaanisha kuwa wanadamu wote ni sawa.
OCHA/Yaye Nabo Sène
Msichana mdogo anashikilia ishara inayosema Zo Kwe Zo, wito wa kitaifa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, ikimaanisha kuwa wanadamu wote ni sawa.

Tunatakiwa kusherekea utajiri wa dini zetu na sio chuki: Guterres

Haki za binadamu

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuwakumbuka waathirika wa vitendo vya vurugu zilizotokana na dini au imani, ulimwengu bado unashuhudia ongezeko la kauli za chuki, kutovumiliana, na hata mashambulio ya mwili kwa watu, vikundi au maeneo, sababu ikiwa ni imani yao ya dini au umuhimu wake.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika taarifa ya maadhimisho ya siku hii amesema vitendo vya vurugu mara nyingi huambatana na uvunjifu wa haki za kimsingi kiwemo haki ya uhuru wa mawazo au dhamiri fulani na vyote hivi vinapaswa kubadilika na kuheshimiana.

“Uhuru wa dini au imani ni haki ya binadamu, iliyowekwa katika Hati ya Umoja wa Mataifa na katika Azimio la Ulimwengu la Haki za Binadamu. Leo, haki hii inajaribiwa. Kwa pamoja tujitolee kuweka ahadi ya kubadili tabia hii na kujenga jamii zinazojumuisha zaidi na zenye amani, ambapo  pamoja na utofauti wetu lakini tunatakiwa kusherehekea utajiri ambao unatuimarisha sisi sote.” 

Guterres amesema janga la COVID-19 limeongeza ubaguzi, kuwatenga na kuwanyima taarifa na mara nyingi walengwa wamekuwa ni vikundi vidogo vya jamii ndogo zenye imani tofauti na hii inaongeza zaidi muunganiko wa hatari. 

“Licha ya hatari, waathirika wanaendelea kupaza sauti zao kwa ujasiri mkubwa kutetea haki zao. Nasimama nao na kuwa na mshikamano nao kamili – na kwa juhudi zinazofanywa na asas iza kiraia, jamii na viongozi wa dini katika kuhamasisha kupinga aina yeyote ya kitendo cha vurugu au ubaguzi.” Amesema Guterres

Akitaja juhudi alizofanya Guterres ameseme “Nimefanya jambo hili kuwa moja ya vipaumbele vyangu kwa kufanya mambo kadhaa ikiwemo kupitia mipango mbalimbali kama Wito wa Kutenda Haki za Binadamu, Mkakati wa Umoja wa Mataifa wa Mpango wa utekelezaji juu ya kauli za chuki na Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Maeneo ya dini.”

Nchi zinajukumu la msingi ka kuzuia ubaguzi na vurugu na kulinda haki za binadamu na haki ya kuabudu ya jamii ndogo na kuhakikisha wanaotenda vitendo viovu vya uhalifu wanafikishwa katika vyombo vya sheria na kuchukuliwa hatua stahiki. Wakati huo huo jamii za kimataifa lazima nazo zifanye vitu vya zaidi kusaidia waathika wa matendo hayo mabaya, pamoja na wale wanaofanya kazi kushughulikia visababishi vya kutokuwepo kwa hali ya kuvumiliana na chuki.