Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana lazima washiriki katika kujenga ulimwengu bora, asihi Katibu Mkuu wa UN

Ushiriki hai wa vijana ni kiini cha jamii thabiti na kuzuia vitisho vibaya zaidi dhidi ya  maendeleo endelevu, pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi
ICAN/Lucero Oyarzun
Ushiriki hai wa vijana ni kiini cha jamii thabiti na kuzuia vitisho vibaya zaidi dhidi ya maendeleo endelevu, pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi

Vijana lazima washiriki katika kujenga ulimwengu bora, asihi Katibu Mkuu wa UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Wakati ulimwengu ukiendelea kukabiliwa na janga la Covid-19, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo Alhamis ametaka kuhakikisha ushiriki wa vijana katika kujenga ulimwengu kwa msingi wa ujumuishi, maendeleo endelevu kwa wote. 

Bwana Guterres ametoa wito huo katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani, ambayo huadhimishwa kila mwaka Agosti 12. 

"Vijana wanaongoza juhudi za kujenga maisha bora ya baadaye kwa ubinadamu." Amesema Katibu Mkuu Guterres kupitia ujumbe alioutoa kwa njia ya video.  

Kwa mujibu wa Bwana Guterres, janga la Covid-19 linaonesha jinsi mabadiliko ambayo vijana wanatamani ni muhimu. "Na vijana lazima washiriki kikamilifu katika mabadiliko haya." Amesisitiza 

Mwaka huu, Siku ya Kimataifa ya Vijana ni fursa ya kuangazia suluhisho zinazotengenezwa na wavumbuzi wachanga na wavumbuzi kushughulikia upungufu katika mifumo ya chakula. 

Lakini Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameonya kuwa vijana hawatafanya peke yao na kwamba wanahitaji washirika "ambao wanahakikisha kuwa wanashauriwa, wamejumuishwa na wanaeleweka". 

Tamasha la ubunifu 

Ili kuadhimisha siku hii ya vijana, Ofisi ya Mjumbe wa Katibu Mkuu kwa ajili ya vijana, imeandaa Tamasha kwa jina #YouthLead kuhusu uvumbuzi kwa siku mbili yaani leo Alhamisi na Ijumaa. Siku hii inahusu kusherehekea suluhisho za ubunifu zilizoongozwa na vijana kwa kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu na kupona mbele ya janga la Covid-19. 

TAGS: Siku za UN, Covid-19, Siku ya vijana duniani, Antonio Guterres, SDGs