Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN inafuatilia uchaguzi mkuu nchini Zambia

Debe la kura
Photo: isietn
Debe la kura

UN inafuatilia uchaguzi mkuu nchini Zambia

Amani na Usalama

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema anafuatilia kwa karibu uchaguzi mkuu nchini Zambia unaofanyika leo tarehe 12 Agosti 2021.

Kupitia kwa taarifa iliyotolewa na msemaji wake Stéphane Dujarric mjini New York, nchini Marekani Katibu Mkuu Guterres amesema “natoa wito kwa wananchi wote wa Zambia, haswa wagombea wote na viongozi wa vyama vya siasa kuhakikisha mnafanya sehemu yenu katika kuweka mazingira yanayofaa kwa uchaguzi kuaminika, kujumuisha watu wote na kuwa na uchaguzi wa amani.”

Katibu Mkuu huyo ameahidi Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana na serikali pamoja na wananchi wa Zambia katika kufikia malengo hayo. 

Jumla ya wagombea 16 ailiwemo rais wa sasa wa nchi hiyo Edgar Lungu wanawania kiti hicho cha urais na iwapo hakuna mgombea atakaye fikisha jumla ya asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa, Zambia itaingia katika duru ya pili ya uchaguzi.