Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taliban waanzisha utaratibu wao katika maeneo wanayoyakalia Afghanistan, watetezi wa haki walaani

IOM inasaidia familia zilizofurushwa nchini Afghanistan, ikitoa makazi ya dharura na ulinzi.
IOM/Mohammed Muse
IOM inasaidia familia zilizofurushwa nchini Afghanistan, ikitoa makazi ya dharura na ulinzi.

Taliban waanzisha utaratibu wao katika maeneo wanayoyakalia Afghanistan, watetezi wa haki walaani

Haki za binadamu

Ghasia zinazofanywa na Taliban dhidi ya jamii zilizo chini ya udhibiti wao nchini Afghanistan zimelaaniwa na mshirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ikiwemo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHRC na shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM.

Kamishia Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet, ambaye leo Jumanne ameunga mkono kurejea katika mazungumzo ya amani huko Doha, amesema katika taarifa kwamba kulikuwa na hofu kote Afghanistan, ambayo ilikuwa imesababisha watu kukimbia makazi yao. 

Wanawake wamechapwa viboko na kuuawa katika maeneo yaliyotwaliwa na kundi la Taleban lenye msimamo mkali, wakati waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu pia wameshambuliwa na kuuawa, Bi Bachelet amesema. 

Ripoti za ukiukaji wa haki ambazo "zinaweza kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu" zimeibuka, pamoja na "ripoti zenye kushitusha sana" za uuaji wa wanajeshi wa serikali wanaojisalimisha. Tangu tarehe 9 Julai katika miji minne pekee - Lashkar Gah, Kandahar, Herat na Kunduz takribani raia  

Siku ya Jumatatu Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF pia liliripoti kuongezeka kwa kasi kwa ukiukaji wa haki dhidi ya watoto nchini Afghanistan, kufuatia vifo vya watoto 27 nchini humo katika saa 72 zilizopita, na watoto 136 walijeruhiwa. Lakini "takwimu halisi inaweza kuwa kubwa zaidi," kwani "hawa ni waathirika ambao tumeweza kuwaorodhesha." Amesema Bi Bachelet. 

Kufikia sasa, Taliban imeshika vituo vya utawala 192 vya wilaya huko Afghanistan, imeshambulia miji mikuu ya mkoa na inasemekana imeshikilia miji mikuu sita ya mkoa huko Nimroz, Jawzjan, mkoa wa Kunduz, Takhar na Sar-e-Pul. 

‘Kuishi kwa hofu’ 

Hii leo mjini Geneva,Uswisi msemaji wa Kamishna Mkuu Bachelet, Ravina Shamdasani, amesema kuwa watu waliogopa kwamba Taliban itafuta faida za haki za binadamu za miongo miwili iliyopita, wakati vikosi vya Marekani na vya kimataifa vikiwa vimekamilisha kujiondoa kwao Afghanistan. 

Katika Mkoa wa Balkh, "mwanaharakati wa haki za wanawake amepigwa risasi na kuuawa kwa kukiuka sheria", ameongeza Bi Shamdasani. OHCHR pia imekuwa ikipokea ripoti za "mauaji, mashambulio dhidi ya maafisa wa serikali wa sasa na wa zamani na wanafamilia wao, uharibifu wa nyumba, shule na kliniki na utapanyaji wa idadi kubwa ya vilipuzi vya kujitengenezea," katika maeneo ambayo tayari yamekamatwa na Taliban na katika maeneo yanayoshindaniwa. 

Nusu ya idadi ya watu Afghanstan wako hatarini  

Mkuu wa Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM hii leo Jumanne, naye pia ameeleza wasiwasi wake juu ya athari za mzozo wa Afghanstan kwa watu waliohamishwa, na wale wanaosafiri, pamoja na waliorejea. 

Na zaidi ya watu milioni 5 tayari wamekimbia makazi yao, zaidi ya 359,000 hadi sasa mwaka huu na idadi kubwa ya waliorejeshwa bila hati, yaani takribani Waafghanistan 680,000 wamerudi katika miezi saba ya kwanza ya mwaka huu, kulingana na Timu ya Ufuatiliaji wa Mipaka ya Kurugenzi ya Wakimbizi na Kurudishwa nyumbani, DoRR. 

Mkurugenzi Mkuu wa IOM, António Vitorino alisema kuwa pamoja na nchi hiyo kuwa "katika lindi la wimbi la tatu la COVID-19 na ukame mkali," karibu nusu ya idadi ya watu wa Afghanistan wanahitaji msaada wa dharura, na mahitaji mengine yanatarajiwa kuongezeka.