Je wajua nyumba ijengwe vipi ihimili mabadiliko ya Tabianchi?

31 Julai 2021

Muongo uliopita ulitajwa kuwa wenye viwango vya juu vya joto zaidi katika historia. Majanga yakiwemo moto wa nyika, mafuriko na vimbunga vinazidi kuongezeka huku viwango vya gesi chafuzi vikiwa ni asilimia 62 zaidi tangu wakati mazungumzo kuhusu mabadiliko ya tabianchi yalipoanza mwaka 1990.

Ushahidi uko wazi kuwa tuko mbioni kuishi kuambatana na mabadliko ya tabianchi.
Ripoti mpya ya shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP inaonesha jinsi nyumba zinaweza kujengwa hasa kwenye nchini zinazoendelea
Hebu tumulike njia tano za ujenzi wa majengo yanayoweza kuhimili mabadiliko ya tabianchi kama ilivyochapishwa katika wavuti wa UNEP.

Kujenga kwa kuzingatia viwango vya joto

Makazi haya ya kuhamia waathirika wa mabadiliko ya tabianchi katika eneo la Nakai,jimbo la Khammoune nchini Lao.
World Bank/Stanislas Fradelizi
Makazi haya ya kuhamia waathirika wa mabadiliko ya tabianchi katika eneo la Nakai,jimbo la Khammoune nchini Lao.

Utafiti unaonesha kuwa ifikapo mwaka 2050 watu bilioni 1.6 wanaoishi ndani ya zaidi miji 970, mara kwa mara watakumbwa  na viwango vya juu vya joto hali ambayo itayaweka maisha ya wakazi wa miji hii katka hatari kubwa.
Lakini mazingira yana suluhu zake. Jamii zinaweza kubuni misitu ya mijini na maeneo yenye miti kupungzua joto mijini  kwa kuwa miti huleta kivuli na hali ya ubaridi.
Miundo ya mijengo pia nayo  inaweza kuchangia kupunguza joto ndani ya majengo. Kwa mfano nyumba zinazojengwa kwa saruji nzito na kwa vifaa vingine vizito hutumiwa China, Chile na Misri kupunguza joto.

Kujenga kwa kuzingatia ukame

Eneo kame
UNEP Cambodia
Eneo kame

Mabadiliko ya tabianchi yameathiri misimu ya mvua kote duniani
Uhifadhi ya maji ya mvua na mifumo inayotumiwa kuyakusanya maji ni njia kuu za kuhifadhi maji wakati wa ukame na kupunguza hatari ya kutokea mafuriko wakati misimu ya mvua nyingi.
Maji yaliyokusanywa yanaweza kuhifadhiwa kwenye matanki na kutumiwa nyumbani wakati wa ukame.
Njia nyingine rahisi ya kukabalina na ukame na mafuriko ni kwa kupanda miti au mimea mingine nje ya majengo. Mizizi ya miti hii husadia maji kufyonzwa kwenye udongo na hivyo hupunguza hatari ya kutokea mafurko.

Kujenga kwa kuzingatia mafuriko sehemu za pwani na kupanda viwango maji ya bahari

Jengo hili pindi mvua ikija na mafuriko linaelea. Jengo liko nchini Bangladesh
Giant Grass
Jengo hili pindi mvua ikija na mafuriko linaelea. Jengo liko nchini Bangladesh

Mwaka 2025 watu milioni 410 walio maeneo ya pwani watakuwa katika hatari ya mafuriko na kuongeza viwango vya maji ya bahari.
Huko Kerala, India nyumba zinazoweza kustahimili mafuriko zinajengwa juu ya nguzo ili kuruhusu maji ya mafuriko kupita chini yake.
Kwenye pwani ya Malaysia nyumba zimeinuliwa mita mbili juu kuruhusu maji kupita na miti kumea  chini yake.
Mbinu moja iliyopendekezwa Bangladesh ni kujengwa nyumba ambayo itakalia nguzo zenye matanki yanayoweza kuelea wakati wa mafuriko.
Jengo hilo linaweza kutumiwa kama kituo cha kijamii na kama makazi ya dharura wakati wa mafuriko.

Kujenga kwa kuzingatia vimbunga na upepo mkali

Nyumba za kuhimili vimbunga huko nchini Ufulipino
Rappler.com
Nyumba za kuhimili vimbunga huko nchini Ufulipino

Vimbunga na mawimbi vinatarajiwa kutokea mara kwa mara kufuatia mabadiliko ya tabianchi.
Vinaweza kuathiri majengo kwa njia nyingi kama vile kwa kung’oa mapaa na hata kuharibu misingi ya majengo.
Miundo ya mapaa huwa na umuhimu mkubwa. Uthabiti kutoka msingi wa nyumba hadi kwenye paa ni kati ya njia za kuhakikisha mapaa yanastahimili upepo.

Kujenga kwa kuzingatia baridi

Uwekaji wa mabomba ya kuvuna mvua kutoka kwenye paa za nyumba nchini Tanzania.
UNEP
Uwekaji wa mabomba ya kuvuna mvua kutoka kwenye paa za nyumba nchini Tanzania.

Hii inahusu kujengwa kwa namna ambayo nyumba inaweza kupata joto na kuhifadhi joto la ndani.
Mapaa, kuta na madirisha vinaweza kujengwa kwa namna ambayo vitazuia kupotea kwa joto .
Majengo pia yanaweza kujengwa wa kwa njia ambayo yatakuwa rahisi kumulikwa na jua pia kuta zinastahili kupakwa rangi nyeusi.
Mapaa yanayoweza kusaidia mimea kumea juu yake hutumiwa kwenye miji mingi kote duniani na huonekana kuwa suluhu kwa kuleta ubaridi msimu wa joto na joto wakati wa msimu wa baridi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter