Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fahamu dalili na mengi kuhusu chanjo-homa ya ini

Mhudumu wa afya akiwa na chanjo dhidi ya homa ya ini.
Picha: UNICEF/Shehab Uddin
Mhudumu wa afya akiwa na chanjo dhidi ya homa ya ini.

Fahamu dalili na mengi kuhusu chanjo-homa ya ini

Afya

Katika kuangazia siku ya homa ya ini duniani iliyoadhimishwa tarehe 28 mwezi huu wa Julai ili kuchagiza hatua za kutokomeza ugonjwa huo ili usiwe tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030.

Jambo lililo dhahiri ni kwamba licha ya kwamba ugonjwa huu unaua lakini haueleweki. Katika sehemu hii ya pili ya mahojiano ya Grace Kaneiya na Muuguzi Daniel Otieno wa kitengo cha magonjwa ya kuambukiza katika hospitali kuu ya taifa ya Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya, wanamulika dalili za ugonjwa wa homa ya ini. Muuguzi Otieno anasema dalili ya kwanza ambayo mtu aliye na ufahamu wa  masuala ya afya atagundua ni, “rangi ya manjano kwneye macho kwa kawaida na ngozi pia huenda ikawa na rangi ya manjano au nyekundu isiyo ya kawaida, afya ya mtu pia inadhoofika, uchovu wa mwili, kizunguzungu na kujikuna.”

Kuhusu chanjo muuguzi Otieno amesema kuna chanjo inayotolewa kwa ajili ya kinga dhidi ya homa ya ini hususan kwa wafanyakazi wa afya kwani hao wakao katika hatari ya kukumbana na ugonjwa huo. Ameongeza kwamba kwa kawaida watu wengi hawafahamu kuhusu chanjo hii na hivyo hio inachangia katika kuenea kwa ugonjwa.

Soundcloud

Kwa upande wa watoto, chanjo dhidi ya homa ya ini ipo katika orodha ya chanjo ambazo zimepitishwa kwa mtoto kupata pamoja na chanjo zingine lakini, “licha ya kwa mtoto anapokea chanjo hii lakini iwapo atakumbana na chemi chemi za virusi au kudungwa kwa sinadano ya mgonjwa wa homa ya ini basi atapata ugonjwa huo, kwani chanjo kama zilivyo chanjo zingine ni kwa ajili ya kujenga kinga ya mwili.”

Kuhusu changamoto za kukabiliana na homa ya ini, muuguzi Otieno amesema ukosefu wa taarifa kwa umma ni changamoto, “ugonjwa huu haujapatiwa kipaumbele kama virusi vya ukimwi,VVU na watu wengi hawajui kama ugonjwa upon a kwamba unasambaa haraka hata kuliko VVU.” Hilo ni dhahiri hata wakati wagonjwa wanafika pale hospitalini kwana hawaelewi ugonjwa walio nao na njia za kuzuia hususan kusambaa kwa watu wengine. Aidha muuguzi Otieno ameongeza, “vifaa vya kupima ni vya gharama ya juu na hivyo haipatikani kwa mtu wa kawaida isitoshe gharama ya kuangalia mgonjwa ni ya juu kwa sababu mgonjwa hapaswi kutangamana na watu."

Kwa kuhitimisha muuguzi Otieno ametoa wito kwa serikali, “kuelimisha jamii zaidi kuhusu ugonjwa wa homa ya ini kwamba upon a kumakinika ili kujikinga kutokana na ugonjwa wa homa ya ini.”