Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kasi ya kupeleka chanjo za COVID-19 barani Afrika yaongezeka

Chanzo zilizotolewa kwa Tanzania kwa msaada wa Marekani kupitia mpango wa Umoja wa Mataifa wa kusaka chanjo za Corona au COVID-19, COVAX, na ziliwasili tarehe 24 Julai 2021.
UNICEF/Daniel Msirikale

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, kanda ya Afrika limesema sasa kuna kasi kubwa ya kupeleka shehena za chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 barani Afrika, wakati huu ambao bara hilo limeshuhudia wiki ya pili ya ongezeko kubwa la maambukizi ya ugonjwa huo.

Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshidiso Moeti amesema hayo leo mjni Brazaville, Jamhuri ya Congo wakati wa mkutano kwa njia ya mtandao na viongozi wa kituo cha Afrika cha kudhibiti magonjwa, ACDC.

Waziri wa Afya nchini Tanzania Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza baada ya kuwasili kwa chanjo za COVID-19 jijini Dar es salaam tarehe 24 Julai 2021.
UNICEF/Daniel Msirikale
Waziri wa Afya nchini Tanzania Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza baada ya kuwasili kwa chanjo za COVID-19 jijini Dar es salaam tarehe 24 Julai 2021.

"Wiki iliyopita Afrika imepokea takribani dozi milioni 4 za chanjo dhidi ya COVID-19 ikilinganishwa na dozi 245,000 zilizosafirishwa kutoka bohari ya mfumo wa Umoja wa Mataifa wa usambaji wa chanjo hizo, COVAX katika kipindi chote cha mwezi uliopita wa Juni," amesema Dkt. Moeti.

Miongoni mwa nchi zilizopokea chanjo hivi karibuni ni Tanzania ambayo kupitia COVAX na kwa msaada wa Marekani imepokea dozi zaidi ya milioni 1 za chanjo aina ya Johnson & Johnson.

Lengo la COVAX ni kusambaza dozi milioni 520 kwa Afrika ifikapo mwisho wa mwaka huu wa 2021, chanzo zinazosambazwa kupitia mfuko wa wadhamini wa Muungano wa Afrika AU wa upataji wa chanjo, AVAT.

Inakadiriwa kuwa ifikapo mwezi Septemba, kila mwezi chanzo milioni 10 zitakuwa zinasambazwa Afrika.

Mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini Benin akipatiwa chanjo ya COVID-19 kwenye mji mkuu Cotonou,
UNICEF/Yannick Folly
Mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini Benin akipatiwa chanjo ya COVID-19 kwenye mji mkuu Cotonou,

Hadi sasa takribani chanjo milioni 79 zimewasilishwa Afrika na watu milioni 21 wamepatiwa chanjo saw ana asilimia 1.6 ya idadi ya watu barani humo wenye umri wa kupatiwa chanjo.

Nchi za kipato cha juu zenyewe zimetoa mara 61 ya kiwango hicho cha chanjo ikilinganishwa na nchi maskini.

Ili kupatia chanjo asilimia 30 ya wakazi wa Afrika ifikapo mwaka 2021, bara hilo linahitaji dozi milioni 820 kwa chanzo za dozi mbili mbili.

Chanjo ya Johnson & Johnson ndiyo inayotolewa mara moja lakini Prifzer, Modern ana AstraZenaca zinatolewa dozi mbili mbili.

"Tunaona mwanaga sasa katika upelekaji chanjo Afrika, lakini nasihi nchi zenye ziada zipeleka chanjo kwa Afrika. Nasihi nchi za Afrika nazo zichangamke na ziwe tayari kwa kuwa naona ukame wa chanjo sasa unakaribia kumalizika," amesema Dkt. Moeti.