Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msemo wa ‘mfundishe mtu uvuvi badala ya kumpatia samaki’ wadhihirika Sudan Kusini

Timu ya uhandisi kutoka Thailand, HMEC, inayofanya kazi kwa pamoja na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Sudan Kusini, UNMISS imepatia wakazi wa eneo la Yei mjini Juba mafunzo ya kilimo cha mazao ya chakula sambamba na mapishi kama njia mojawapo
UN Photo/Nektarios Markogiannis
Timu ya uhandisi kutoka Thailand, HMEC, inayofanya kazi kwa pamoja na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Sudan Kusini, UNMISS imepatia wakazi wa eneo la Yei mjini Juba mafunzo ya kilimo cha mazao ya chakula sambamba na mapishi kama njia mojawapo ya kujitegemea katika chakula

Msemo wa ‘mfundishe mtu uvuvi badala ya kumpatia samaki’ wadhihirika Sudan Kusini

Amani na Usalama

Tumu ya uhandisi kutoka Thailand, HMEC, inayofanya kazi kwa pamoja na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Sudan Kusini, UNMISS imepatia wakazi wa eneo la Yei mjini Juba mafunzo ya kilimo cha mazao ya chakula sambamba na mapishi kama njia mojawapo ya kujitegemea katika chakula.

Eneo la Yei mjini Juba nchini Sudan Kusini, walinda amani kutoka Thailand wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS wakiendesha mafunzo ya mapishi ya chakula bora kutokana na mazao waliyopanda kwenye mashamba darasa hapa Yei. 

Walinda amani hawa ni wahandisi na wanatumia filosofía ya mfalme wa Thailand ya kujitosheleza binafsi kwa chakula badala ya kuwa tegemezi.waliendesha mafunzo mara mbili kuhusu kilimo na usindikaji wa mazao ambayo wanapanda hapa ikiwemo yaliyozoeleka kama vile bamia, pamoja na mengine mapya kutoka Thailand. 

Jaak Buom Gathuak, mkimbizi wa ndani ni miongoni mwa wanufaika na anasema, “hali ya Sudan Kusini ni mbaya sana kwa sababu hakuna chakula cha kutosha kwa kuwa kilimo hakiwezekaniki. Hatulimi tena. Nilipopata mafunzo na kuanza kilimo, nilipata ufahmau wa jinsi ya kulima na sasa nina uwezo wa kulima na vile vile kufundisha wengine.” 

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limeratibu mafunzo haya ambapo Victor Onenchan, Mkuu wa ofisi ndogo ya FAO anasema, “Kama FAO tunashukuru sana kwa yeyote anayechangia kutokomeza njaa duniani. Ni sehemu ya malengo ya maendeleo endelevu. Juhudi zetu ni kuona njaa inatokomezwa duniani.” 

Mradi umekabidhiwa kwa jeshi la polisi nchini Sudan Kusini ambalo lilisaidia kuandaa mashamba darasa. 

Ingawa kikundi cha wahandishi kimesalia miezi mitatu kufungasha virago, na jukumu lao kubwa ni masuala ya uhandisi, bado kinasaidia kuangazia maendeleo ya mradi huo ya kufanikisha kujitegemea ambapo Kamanda wa kikosi hicho cha uhandisi Luteni Kanali Kaisin Sasunee anasema, “Ingawa kikundi chetu ni kidogo sana ndani ya UNMISS, tunajaribu kuendeleza na kusaidia jamii ili nchi yao iwe na mustakabali mzuri. Nimemfundisha Junubi jinsi ya kuvua samaki kwa maisha yake yote badala ya kumpatia samaki wa siku moja.”