Ikiwa tutapuuza changamoto na mahitaji ya watu wa vijijini katika nchi maskini tutashindwa - IFAD 

27 Julai 2021

Mkutano wa utangulizi kuhusu mifumo ya chakula ukiendelea mjini Roma, Italia, Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo, IFAD limetoa wito wa mabadiliko kadhaa muhimu katika mifumo ya chakula, ikiwemo kujitolea kufadhili na pia dhamira ya kisiasa kuhakikisha watu wa vijijini wanawezeshwa kwa namna mbalimbali vinginevyo lengo la kuwa mifumo endelevu ya chakula duniani litashindwa.

Ni Rais wa IFAD Gilbert Houngbo  akiweka wazi mtazamo wa shirika hilo la Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo kwa kusema kuwa ikiwa ulimwengu utapuuza, “changamoto na mahitaji ya watu wa vijijini katika nchi maskini zaidi duniani, majaribio ya kuunda mifumo ya chakula yenye usawa na endelevu yatashindwa. ” 

Wito wa IFAD unazingatia hali halisi duniani katika maeneo maskini  kama nchini Pakstani anakoishi Shabana Bibi mwenye mwanamke mwenye umri wa miaka 35 ambaye  

Anapata shida ya kipato kutokana na shughuli yake ya kuvuna ngano na kuokota pamba katika eneo la Bahawalpur. Pia anajihusisha na kushona ili aweze kulipia mahitaji lakini mara nyingi pesa anazopata bado hazitoshi na watoto wake wanapata njaa.Shabana anasema, "Kila kitu ni kigumu, lakini hatuna chaguo jingine zaidi ya bidii ili kulea watoto." 

Shabana na familia yake wanatumai sauti yao itasikilizwa na viongozi wanaohudhuria ulioanza jana Julai 26 na unaendelea hadi kesho Julai 28 mjini Roma Italia ndio maana Shabana anasema, “Nataka kuwaomba viongozi wa ulimwengu kudhibiti bei za bidhaa za chakula. Ninaomba viongozi wa ulimwengu tafadhali waondoe umaskini.” 

Kwenye Mkutano huo wa wa Awali wa Mifumo ya Chakula, IFAD imejiunga na maafisa wa  serikali, kampuni, mashirika ya maendeleo, wakulima na asasi za kiraia kujadili njia za kubadilisha jinsi kilimo kinavyofanyika, usindikaji, kuuza na kula chakula ili kuifanya iwe zaidi endelevu na yenye usawa. Mkutano wa mapema unakusudia kuanzisha dira ya pamoja, kuzindua ahadi na kuhamasisha ufadhili na ushirikiano. 

IFAD inahakikisha wakulima na wazalishaji wa vijijini watasikilizwa. Jukwaa la Sauti Vijijini linawapa wazalishaji wa vijijini kama Shabana nafasi ya kuweka wazi wasiwasi wao hadhira pana. Rais wa IFAD Bwana Houngbo, anasisitiza akisema, "ikiwa unataka kurekebisha mifumo ya chakula, sikiliza watu wanaofanya kazi ndani ya mifumo hiyo. Wakulima wadogo vijijini huzalisha karibu theluthi moja ya chakula chetu cha ulimwengu, lakini mara nyingi hupokea kidogo kwa ajili ya juhudi zao na wanaachwa katika hatari.”. 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter