Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima ni 'uhai wa mifumo yetu ya chakula' - Naibu Katibu Mkuu wa UN 

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed alipokutana na wanaewake wakulima katika soko la wakulima Circo Massimo, Rome.
UN Photo.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed alipokutana na wanaewake wakulima katika soko la wakulima Circo Massimo, Rome.

Wakulima ni 'uhai wa mifumo yetu ya chakula' - Naibu Katibu Mkuu wa UN 

Wanawake

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J Mohammed hii leo Jumamosi amekutana na wanawake wakulima katika soko la wakulima huko Circo Massimo, Roma, kabla ya Mkutano wa awali wa kuhusu mfumo endelevu wa chakula uliwenguni unaofanyika wiki ijayo. 

Makumi kadhaa ya mabanda yamewekwa karibu na eneo la eneo la mkutano ambapo wakuu wa nchi na wajumbe watakusanyika kuanzia  Jumatatu kujadili njia za kubadilisha mifumo ya chakula kukabiliana na  

Umoja wa Mataifa na maafisa wa serikali wametembelea soko hilo kukutana na wakulima kabla ya kutoa heshima kwa wazalishaji, hasa wanawake, kwa jukumu lao kuu katika mifumo ya chakula. 

"Wakulima ni uhai wa mifumo yetu ya chakula", amesema Bi Mohammed akiongeza kuwa, "kuelewa mahitaji yao na changamoto wanazokabiliana nazo husaidia kuhakikisha kuwa suluhisho zinazojitokeza zinafaa kwa kusudi hilo.” 

Tukio hili la siku tatu litawaleta pamoja vijana, wakulima, watu wa Asili, asasi za kiraia, watafiti, sekta binafsi, viongozi wa sera na mawaziri wa kilimo, mazingira, afya, lishe na fedha, kati ya wahusika wengine muhimu.