Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maji yashika usukani katika uharibifu duniani 1971 hadi 2019

Mataifa ya Kusini na Mashariki mwa Afrika yanaendelea kukabiliwa na mafuriko, ukame na matukio mengine ya mabadiliko ya hali ya hewa katika miaka ya karibuni
UNDP/Arjen van de Merwe
Mataifa ya Kusini na Mashariki mwa Afrika yanaendelea kukabiliwa na mafuriko, ukame na matukio mengine ya mabadiliko ya hali ya hewa katika miaka ya karibuni

Maji yashika usukani katika uharibifu duniani 1971 hadi 2019

Tabianchi na mazingira

Majanga yahusiano na maji yameongoza katika orodha ya matukio 10 ya majanga yaliyogharimu uhai na uchumi duniani katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, imesema ripoti iliyotolewa leo mjni Geneva, Uswisi na shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa duniani, WMO.

 

Tweet URL

Dhoruba, ukame, mafuriko na viwango vya joto kupita kiasi vimeongoza katika orodha hiyo ya ripoti iliyopatiwa jina Ramani ya vifo na hasara za kiuchumi  kutokana na hali ya hewa, tabianchi na maji kupindukia kuanzia mwaka 1970 hadi 2019.

Ikichambua idadi ya vifo, ukame pekee ulisababisha watu 650,000 duniani kote kufariki dunia, pili ni dhoruba watu 577,232, mafuriko watu 58,700 na joto kupindukia vifo 55, 736.
Kwa upande wa kiuchumi, dhoruba zilisababisha hasara yad ola bilioni 521 huku mafuriko yaligharimu uchumi dol abilioni 115 duniani kote kuanzia mwaka 1971 hadi 2019.

Hasa kubwa zaidi ya kiuchumi ilikumba bara la Ulaya, mathalani mafuriko ya mwaka 2002 nchini Ujerumani yalisababisha hasara ya dola bilioni 16.48.

Mabadiliko ya Tabianchi

Uchambuzi huo unaonesha kuwa hali ya hewa, tabianchi na majanga yasababishwayo na maji yanaongeza viwango vyake vya uharibifu kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Akifafanua ripoti hiyo, Katibu Mkuu wa WMO Profesa Petteri Taalas amesema, “hasara za kiuchumi na kupoteza uhai wa binadamu ziliakisiwa vyema wakati wa mvua kubwa na mafuriko yaliyokumba eneo la kati la Ulaya na China wiki iliyopita. Viwango vya kuvunja rekodi vya mkondo joto huko Amerika ya Kaskazini vyote vinahusiana dhahiri na ongezeko la joto duniani.”

 

Ameongeza kuwa kadri joto linaongezeka duniani na anga linapata unyevunyevu ndivyo mvua zaidi inanyesha wakati wa vimbunga na vile vile hatari ya kuweko kwa mafuriko.

Waokoaji wakisaidia kumuopoa mwanakijiji aliyekumbwa na mafuriko kwenye mji wa Xingyang jimboni Henan nchini China
China Fire and Rescue
Waokoaji wakisaidia kumuopoa mwanakijiji aliyekumbwa na mafuriko kwenye mji wa Xingyang jimboni Henan nchini China

 

“Hakuna nchi iwe tajiri au maskini ina kinga hapa. Mabadiliko ya tabianchi yamefika na yako hapa. Ni vema kuwekeza zaidi katika hatua kwa tabianchi na njia moja ya kufanya hivyo ni kuimarisha mifumo yetu ya kutoa maonyo mapema dhidi ya majanga,” amesema Profesa Talaas.

Kitabu hicho cha ramani ya majanga kitachapishwa kuelekea mkutano mjadala mkuu wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka huu na ni moja ya machapisho ya kuwawezesha viongozi na watunga sera kuwa na taarifa za kisayansi kuhusu hali ya hewa na tabianchi.