Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN ina furaha kuwa mchezaji mwenza wa Olimpiki; Guterres

Michezo ya olimpiki kuanza rasmi Julai 23, 2021.
© 2021 - IOC/Yuichi Yamazaki
Michezo ya olimpiki kuanza rasmi Julai 23, 2021.

UN ina furaha kuwa mchezaji mwenza wa Olimpiki; Guterres

Masuala ya UM

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa ujumbe kwenye ufunguzi wa michuano ya Olimpiki mjini Tokyo,Japan ambapo ameeleza michuano hiyo inaleta ubinadamu, kuwaunganisha watu pamoja, kuonesha talanta zao na uvumiliv

“Pamoja na uwepo wa janga la Corona lakini wanamichezo wameonesha uvumilivu, sote tupo kwenye maombolezo ya wapendwa wetu kutokana na janga la COVID-19. kila mwanamichezo aliyeko Tokyo ameshinda vizuizi vikubwa na alionesha dhamira ya dhati ya kushiriki katika michuano hiyo” amesema Guterres katika video yake iliyooneshwa wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo.

Amesema ikiwa watu wote duniani watatumia nguvu kama walizotumia wanamichezo walioko Japan basi dunia itafanikiwa kutatua changamoto nyingi.

“Amani, ulimwengu ulio msafi, wakijani na unaostawi, ulimwengu bora wenye usawa uliojikita kwenye kusaidia wenye uhitaji zaidi na ambao hautaki hata mtu mmoja abaki nyuma. Embu tukimbie pamoja kufikia ulimwengu wa aina hiyo.”

Guterres amehitimisha hotuba yake hiyo fupi akiwatakia wachezaji wote mashindano mema, na kusema Umoja wa Mataifa unayo heshima kubwa kuwa mchezaji wenza katika kila hatua.