Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tukiwa na maeneo ya faragha, wanawake wengi zaidi wataendesha malori- Maissata 

Vifaa vya hali ya juu kwa ajili ya kuvuka mipaka.
Vigen Sargsyan/World Bank
Vifaa vya hali ya juu kwa ajili ya kuvuka mipaka.

Tukiwa na maeneo ya faragha, wanawake wengi zaidi wataendesha malori- Maissata 

Ukuaji wa Kiuchumi

Kutana na Maissata Cisse al maaruf Mama Afrika, huyu ni dereva pekee wa malori ya safari ndefu katika ukanda wa Afrika Magharibi akiendesha malori ya mizigo katika nchi za Benin, Burkina Faso, Guinea, Côte d’Ivoire baadhi ya nyinginezo akisema kuwa uboreshaji wa miundombinu ya barabara na tararibu za forodha katika ukanda huo vimekuwa jawabu mujarabu wa kazi yake hiyo aliyoifanya kwa miaka 30 sasa. 

Naitwa Maissata Cisse au Mama Afrika… 

Ndiyo inavyoanza video ya Benki ya Dunia ambapo mwanamke huyo dereva wa malori anasema anaamini ni yeye pekee katika ukanda wa Afrika Magharibi aendeshaye malori ya mizigo ya masafa marefu. 

Akiwa amevalia kitenge, anaendesha lori kwa umakini mkubwa !! 

Anasema anajivunia kuwa mwafrika na kila mkazi wa Afrika ni familia yake. Alipoulizwa kuhusu ubora wa barabara na mchango katika kazi yake amesema.. “Wakati naanza kazi, barabara zilikuwa mbayá. Tulitumia wiki nzima kusafiri kutoka Lome, Togo hadi Ouagadougou [WAGADUGU] Burkina Faso. Kulikuwa na vituo vingi vya ushuru. Lakini siku hizo barabara ni nzuri na ni jambo zuri kweli.” 

Ili kulinda ubora wa barabara hizo, Jumuiya ya kiuchumi na kifedha ya Afrika Magharibi, WEAMU [WEAMU] ilianzisha vituo vya kupima uzito wa malori. “Kila dereva wa lori anapaswa kupima uzito wa lori lake. Ni vizuri kupima ili kutambua uzito unaotakiwa na hivyo kutunza barabara. Kubeba mizigo kupita kiasi si vizuri kwa barabara.” 

Kuna wakati lori lake linapata matatizo, Maissata anaingia chini ya lori na kutengeneza na ndoto yake ni siku moja anunue lori jipya angalau mawili.  

Lakini jambo lingine ni.. « Ili wanawake waweze kufanya kazi hii vizuri, tunahitaji maeneo ya faragha, ili wanawake waweza kujisafi hili ni muhimu. Kama kutakuwepo na usalama, basi wanawake wengi watajiunga na kazi hii. »