Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Mama Mjane anayelea wajukuu wake watatu huko Douala, Cameroon.

Katika wakati huu mgumu wa COVID-19 tusiwape kisogo wajane:Guterres

UN Women/Ryan Brown
Mama Mjane anayelea wajukuu wake watatu huko Douala, Cameroon.

Katika wakati huu mgumu wa COVID-19 tusiwape kisogo wajane:Guterres

Msaada wa Kibinadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameiasa dunia kutowasahau wajane hasa wakati huu wa janga la corona au COVID-19 ambapo wanaume wengi wanaendelea kupoteza maisha na kuwaacha wake zao wakihaha na familia. 

Kupitia ujumbe wake wa siku ya wajane duniani inayoadhimishwa leo Juni 23 Antonio Guterres amesema “Huu ni wakati muafaka wa kuzingatia mwelekeo wa mara kwa mara uliosahaulika wa shida, maisha na hatima ya wajane walioachwa nyuma. Kifo cha mwenzi wakati wowote kinaweza kuwaacha wanawake wengi bila haki ya urithi au mali. Wakati wa janga hasara hizi mara nyingi huongezeka kwa wajane na huambatana na unyanyapaa na ubaguzi.” 


Guterres ameongeza kuwa viwango ambavyo havijawahi kutokea vya kutengwa na changamoto za kiuchumi zilizoletwa na mgogoro wa COVID-19 zinaweza kudhoofisha zaidi uwezo wa wajane wa kujikimu na familia zao, na kuwaternganisha na uhusiano wa kijamii wakati ambao ni wa huzuni kubwa. 
Katibu Mkuu amesisitiza kuwa “Tunapojitahidi kushughulikia COVID-19, serikali lazima zifanye kazi kujumuisha msaada kwa mahitaji ya haraka ya wajane katika mipango ya kichocheo cha fedha, kwa mfano kupitia ufikiaji wa uhamishaji wa kuchangisha pesa.“

Mbali ya hayo amesema dunia inapojitahidi kujikwamua kutoka kwenye janga hili juhudi hizo lazima zifuatwe na mabadiliko ya kimuundo ya muda mrefu, pamoja na kumaliza sheria za kibaguzi zinazowanyima wanawake haki sawa na wanaume na kuhakikisha upatikanaji wa ulinzi wa jamii, ili wanawake wasianze kwa hasara.  
Pia ameongeza kuwa “Tunahitaji takwimu bora, zilizogawanywa kwa minajili ya umri na jinsia, kuhakikisha kuwa wajane wanahesabiwa na kuungwa mkono, sasa na katika siku zijazo.” 


Katika siku hii ya wajane Guterres amehimiza kuwa “Hebu tuimarishe jamii zetu, tahamani ya familia na kuzijenga upya jamii ambazo zinawaunga mkono na kuwasaidia wajane katika kila nyanja.”