Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kifo cha Kaunda kimenishtua na kunisikitisha- Guterres 

Hayati Kenneth Kaunda wakati akiwa Rais wa Zambia alifanya ziara rasmi Umoja wa Mataifa na kuhutubia Baraza Kuu tarehe 15 mwezi Novemba mwaka 1966.
UN

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa na kusikitishwa sana na taarifa za kifo cha Rais wa zamani wa Jamhuri ya Zambia, Kenneth Kaunda. 

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Stephane Dujarric akijibu sawali kuhusu kifo hicho wakati wa mkutano na waandishi wa Habari hii leo mjini New York Marekani Guterres amesema katika wakati huu mkugu wa pengo kubwa “Natuma salamu za rambirambi kwa familia  ya Rais wa zamani, kwa Serikali na watu wa Jamhuri ya Zambia.” 

Ameongeza kuwa  “Kama baba mwasisi wa taifa la Zambia, Rais wa zamani Kaunda alikuwa na mchango mkubwa katika kupanga mkakati wa baada ya uhuru wa nchi hiyo kuelekea demokrasia ya vyama vingi na alikuwa mtu wa kujitolea kwa maslahi ya Afrika.” 

Keneth Kaunda ameaga dunia hii leo akiwa na umri wa miaka 97.