Skip to main content
Karibu Umoja wa Mataifa
Lugha
  • العربية
  • 中文
  • English
  • Français
  • Русский
  • Español
  • Português
  • Kiswahili
  • Nyingine
    • Hindi हिंदी
    • duniani
Umoja wa Mataifa
Habari za UN
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Search the United Nations

Tafuta Zaidi
  • Mwanzo
    • Afrika
    • Amerika
    • Asia Pasifiki
    • Mashariki ya Kati
    • Ulaya
  • Mada
    • Amani na Usalama
    • Ukuaji wa Kiuchumi
    • Msaada wa Kibinadamu
    • Tabianchi na mazingira
    • Haki za bindamu
    • Masuala ya UM
    • Wanawake
    • Sheria na Kuzuia Uhalifu
    • Afya
    • Utamaduni na Elimu
    • SDGs
    • Wahamiaji na Wakimbizi
  • Kwa kina
    • Habari kwa Picha
    • Mahojiano
    • Makala
    • Neno La Wiki
    • Makala Maalum
    • Videos
    • Siku za UN
  • Katibu Mkuu
    • Msemaji wa Katibu Mkuu
    • Taarifa zote
    • Hotuba muhimu
    • Mikutano na wanahabari
    • Safari za kikazi
  • Vyombo vya Habari
    • Video za Umoja wa Mataifa
    • Picha za Umoja wa Mataifa
    • Matukio ya Mikutanoni
    • Usajili kwa wanahabari
    • Webtv
  • Mwanzo
    • Afrika
    • Amerika
    • Asia Pasifiki
    • Mashariki ya Kati
    • Ulaya
  • Mada
    • Amani na Usalama
    • Ukuaji wa Kiuchumi
    • Msaada wa Kibinadamu
    • Tabianchi na mazingira
    • Haki za bindamu
    • Masuala ya UM
    • Wanawake
    • Sheria na Kuzuia Uhalifu
    • Afya
    • Utamaduni na Elimu
    • SDGs
    • Wahamiaji na Wakimbizi
  • Kwa kina
    • Habari kwa Picha
    • Mahojiano
    • Makala
    • Neno La Wiki
    • Makala Maalum
    • Videos
    • Siku za UN
  • Katibu Mkuu
    • Msemaji wa Katibu Mkuu
    • Taarifa zote
    • Hotuba muhimu
    • Mikutano na wanahabari
    • Safari za kikazi
  • Vyombo vya Habari
    • Video za Umoja wa Mataifa
    • Picha za Umoja wa Mataifa
    • Matukio ya Mikutanoni
    • Usajili kwa wanahabari
    • Webtv
 

Sajili

Kabrasha la Sauti

Mfuko wa usaidizi wa dharura wa UN, CERF umesaidia kusambaza misaada ya dharura ya kibinadamu ikiwemo chakula kama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ambako mgogoro usiomalizika umeacha wananchi bila mahitaij  ya kimsingi
MINUSCA/Nektarios Markogiannis
Mfuko wa usaidizi wa dharura wa UN, CERF umesaidia kusambaza misaada ya dharura ya kibinadamu ikiwemo chakula kama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ambako mgogoro usiomalizika umeacha wananchi bila mahitaij ya kimsingi

Dola Milioni 135 zatolewa na UN kusaidia wanaokabiliwa na Njaa

15 Juni 2021
Msaada wa Kibinadamu

Umoja wa Mataifa umetoa dola milioni 135 kutoka kwenye Mfuko wake wa dharura (CERF) ili kuongezea kwenye shughuli za kibinaadamu katika nchi 12 barani Afrika, Amerika na Mashariki ya Kati, amesema Mratibu wa Mfuko huo Bwana Mark Lowcock akiwa mjini New York, Marekani.

 

Amesema fedha hizo zimetolewa kufuatia takwimu zilizotolewa wiki iliyopita, zikionesha zaidi ya watu 350,000 wanakabiliwa na njaa  katika mji wa Tigray Ethiopia, na tishio la njaa katika nchi ya Burkina Faso, Kusini mwa Madagascar, kaskasini- Mashariki mwa Nigeria, Sudan Kusini na Yemen.
Mark Lowcock ameongeza kuwa “Njaa inaendelea kuongezeka maeneo kadhaa hivi sasa, mgawanyo huu wa fedha zilizotolewa unaweza kuleta tofauti kati ya maisha na kifo, kwa mamilioni ya watu wanaotegemea msaada ili kuishi. Msaada utatoa vitu muhimu kama maji safi, malazi na chakula kwa watu walio na uhitaji sana wakati huu.”
Ameeleza fedha hizo zitagawanywa kwenye mashirika ya misaada kama ifuatavyo, Syria itapata dola milioni 20, Jamhuri ya Kidemokrasia Congo -DRC dola milioni 20, Ethiopia zilielekezwa mkoa wa Tigray Dola milioni 13.
Nchi za Afghanistan, Nigeria na Sudan Kusini kila moja itapata dola milioni 11 kusaidia shughuli za misaada. Na fedha zilizosalia zitapelekwa Madagascar dola milioni 8, Venezuelea dola milioni 7, Chad dola Milioni 7, Burkina Faso dola Milioni 7, Cameroon dola Milioni 5, na Msumbiji dola milioni 5. Miradi ya kusaidia watu wenye ulemavu imetengewa dola milioni 10. 
“Mahitaji ya kibinadamu yanaendelea kuzidi misaada ya kibinadamu inayotolewa, na sio mizozo yote inayopewa uangalifu sawa wa uhitaji wa kifedha, na ndio maana mfuko huu kwa sasa ni muhimu kupita wakati mwingine wowote sababu unakuwa nyenzo muhimu ya kurekebisha usawa kwa kuhakikisha kuwa kazi muhimu ya misaada inaendelea kila mahali.” Amesema Lockcock. 
Tangu kuanzishwa kwa mfuko huu wa dharura mwaka 2005 ambao unapokea mchango wa hiyari kutoka nchi 129 pamoja na wadau wengine wa misaada, mamilioni ya watu wamepata msaada wa dola za Kimarekani bilioni 7 kwenye zaidi ya nchi 100 duniani, hii ikijumlisha zaidi ya dola bilioni 2.3 kwenye mizozo iliyopata ufadhili kidogo tofauti na uhitaji wake . 
 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter
misaada|njaa

Taarifa Zihusianazo

Watu milioni mbili na nusu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ( CAR)wanakabiliwa na njaa

Wanaotegemea msaada wa kibinadamu wana hali tete

WFP imelazimika kupunguza mgao wa chakula Sudan Kusini na baadhi ya sehemu za  Afrika Mashariki

Ukata wazidisha ongezeko la njaa miongoni mwa wakimbizi:WFP 

Mizozo imesalia kuwa kichocheo kikubwa cha ukosefu wa uhakika wa kupata chakula duniani.

Tubadili mwelekeo wa kukabili uhaba wa chakula- Ripoti

Maktaba

  • Taarifa kwa watangazaji
  • Viunganishi vya Umoja wa Mataifa
  • Angalizo
  • UN Journal
  • Taarifa za Habari
  • Mikutano
  • Maktaba ya Picha na Video
  • Wasiliana nasi

Katibu Mkuu

  • Taarifa zote
  • Safari za kiofisi
  • Kona ya wanahabari
  • Kutoka Twitter ya Katibu Mkuu

Msemaji wa UN

  • Nyaraka zote
  • Muhtasari wa mkutano na wanahabari
  • Maandishi ya mkutano na wanahabari
  • Taarifa kwa wanahabari

Tupate

  • Facebook
  • Twitter
  • YouTube
  • RSS
  • Mawasiliano
  • Rambaza
  • Washirika wetu kwa sasa
Umoja wa Mataifa
Changia
  • Facebook
  • Twitter
  • YouTube
  • Soundcloud
  • Podcast
  • UN Social Media
  • A-Z Site Index
  • Hakimiliki
  • Maswali ya mara kwa Mara
  • Fraud Alert
  • Privacy Notice
  • Kanuni za matumizi
  • Facebook
  • Twitter
  • YouTube
  • SoundCloud
  • Podcast
  • More Socials