Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Kambi ya Cox's Bazar inayohifadhi warohingya nchini Bangladesh.

Hatutoi Taarifa za wakimbizi kwa serikali ya Bangladesh bila ridhaa ya Wakimbizi wenyewe : UNHCR

IOM/Mashrif Abdullah Al
Kambi ya Cox's Bazar inayohifadhi warohingya nchini Bangladesh.

Hatutoi Taarifa za wakimbizi kwa serikali ya Bangladesh bila ridhaa ya Wakimbizi wenyewe : UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR kupitia tarifa yake kwa vyombo vya habari hii leo mjini Geneva Uswisi limesema halikusanyi taarifa za wakimbizi wa Rohingya waliopo Bangladesh na kuipa serikali bila idhini ya wakimbizi wenyewe na iwapo wakimbizi hao watakataa kutoa ruhusa basi watapatiwa mahitaji muhimu kama wale waliokubali bila kubaguliwa kwa aina yeyote. 

 

Tarifa hiyo imefuatia uwepo wa maswali ya kwanini UNHCR inakusanya tarifa za wakimbizi na wanazifanyia kazi gani. 
“UNHCR na mawakala wake wana será iliyowazi inayohakikisha usalama wa tarifa zinazokusanywa wakati wa usajili wa wakimbizi duniani kote.Ukusanyaji wa taarifa za wakimbizi ni muhimu kwani zinasaidia kujua mahitaji ya kila mmoja na kumpatia msaada stahiki, kwa haraka na pia inasaidia kuwaunganisha wanafamilia waliopotezana.”
Wakati UNHCR na serikali ya Bangladesha iliposaini makunaliano ya kubadilishana taarifa Januari 2018, na kufanyakazi kwa pamoja kusajili wakimbizi wa Rohingya, hatua maalum zilichukuliwa kupunguza hatari zinazoweza kujitokeza. 
“Hatua hizo ni pamoja na kulinda takwimu dhidi ya uharibifu au usiyoinidhinishwa, upotezaji wa takwimu bahati mbaya, ufikiwaji wa taarifa bila ruhusa, mabadiliko ya matumizi au usambazaji na aina nyingine yeyote usioidhinishwa. “
Kuhusu iwapo taarifa za ushauri nasaha zinazotolewa na wafanyakazi kwa wakimbizi wanaohitaji taarifa hiyo imesema hizo ni tarifa za siri na hazitolewi kwa serikali.

Wakimbizi wa Rohingya ambao wamewasili Bangladesh wanapatiwa maelekezo na kujaza fomu iwapo wanatoa ridhaa ya tarifa zao kuoneshwa kwa serikali na wanajaza fomu zaif ya mbili kutoa idhina na wale wote wanaokataa tarifa zao zisioneshwe kwa mtu wa tatu basi UNHCR inaheshimu takwa lao na inawapatia elimu kuwahakikishia wote watapata huduma sawa bila aina yeyote ya upendeleo kwa wale waliokubali.