Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya waliotawanywa na volkano DRC wahitaji msaada wa haraka:UNHCR

Vituo vya maji vilivyowekwa na UNICEF kwa wakazi waliopoteza makazi  yao kufuatia mlipuko wa volkano ya Nyiragongo huko Sake jimboni Kivu Kaskazini.
UNICEF/Jean-Claude Wenga
Vituo vya maji vilivyowekwa na UNICEF kwa wakazi waliopoteza makazi yao kufuatia mlipuko wa volkano ya Nyiragongo huko Sake jimboni Kivu Kaskazini.

Maelfu ya waliotawanywa na volkano DRC wahitaji msaada wa haraka:UNHCR

Msaada wa Kibinadamu

Mamia kwa maelfu ya watu waliotawanywa na mlipuko wa volcano wa mlima Nyiragongo Masharki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, sasa wanahitaji msaada wa haraka katika maeneo walikokimbilia na kupata hifadhi kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Flora Nducha anasimulia zaidi 

Paul mwenye ulemavu mmoja wa waathirika wa volcano hiyo ambao walipitia madhila njiani hadfi kuwasili hapa Sake ambapo sasa wanapata hifadhi 

Ingawa maisha yao yako salama lakini wanakabiliwa na mitihani mikubwa kwani wengi wanapata hifadhi katika miji na vijiji vya Jirani ambako wanaishi katika mazingira magumu sana na wengine wakilazimika kulala katika maeneo ya wazi liwe jua , iwe mvua kama anavyothibitisha Jean miongoni mwa wakimbizi ha“Tulishuhudia mvua ya cheche na mawe, kila kitu kiliteketea kabisa. Hapa tunahangaika sana, tunalala nje katika maeneo ya wazi, tunahofia baridi usiku itasababisha tuumwe. Nyumba zetu, nguo, mablanketi, vitanda vyote viliteketea,tulikuwa na kuku na mbuzi na sasa hatuna chochote." 

Maelfu ya watu wamevuka mpaka kuelekea Rwanda kutoka Goma kufuatia mlipuko wa mlima Nyiragongo.
© UNICEF/Olivia Acland
Maelfu ya watu wamevuka mpaka kuelekea Rwanda kutoka Goma kufuatia mlipuko wa mlima Nyiragongo.

UNHCR na washirika wake wanafanyakazi kwa karibu na serikali na wanajitahidi kutoa msaada wa malazi, maji na chakula.  

Lakini fedha zaidi na msaada wa haraka vinahitajika. 

Serikali inawachagiza watu kurejea Goma kwani volcano imetulia na hali imekuwa shwari lakini wengi kama Paul bado wana hofu baada ya

kupoteza kila kitu  "Nilikuwa nimepanga nyuma , siku na yangu sasa sijui kama mwenyenyumba atakuwa ameniwekea nafasi , sijui kwani nilikuwa mpangani.” 

Waathirika wakubwa ni wanawake, watoto na watu wenye ulemavu kama mama Nema “Watu wote wenye ulemavu tuko wengu tunalala mahali pamoja hapa katika shule . Niko na watoto sit ana nina lala nao chini, chakula shida tunakula maran moja tu usiku na wazazi tunagawiwa kopo moja la unga, kopo moja la mchele na kopo mojamoja la maharage." 

UNHCR imeahidi kutowatelekeza wakimbizi hawa huku ikitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kunyoosha mkono kuwasaidia kwani bila msaada maisha yao yako hatarini.