Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Picha ya upande wa Palestina wa Karem Shalom ambako bidhaa zinaingia na kutoka kati ya Israel na Gaza , ambapo sehemu iliteketezwa kwa moto na Wapalestina, na kuathiri uwezo wake wa kusafirisha baadhi ya bidhaa cha chakula ikiwemo pia mafuta ya dharura. 1

UN yalaani mauaji ya mjamzito nchini Palestina

Picha na UN
Picha ya upande wa Palestina wa Karem Shalom ambako bidhaa zinaingia na kutoka kati ya Israel na Gaza , ambapo sehemu iliteketezwa kwa moto na Wapalestina, na kuathiri uwezo wake wa kusafirisha baadhi ya bidhaa cha chakula ikiwemo pia mafuta ya dharura. 1

UN yalaani mauaji ya mjamzito nchini Palestina

Haki za binadamu

Umoja wa Mataifa umelaani vikali mauaji ya mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka 19 aliyeuwawa na mume wake nchini Palestina, na kutoa wito vya vyombo vya usalama vya nchi hiyo kuhakikisha haki inatendeka
 

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, Dr.Luay Shabaneh Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya atu duniani- UNFPA kwa nchi za kiarabu amesema, “ aina hii ya uhalifu mbayá haikubaliki tena. Natoa wito kwa mamlaka kutoa ulinzi na msaada kwa wasichana na wanawake wote kutoka kwa aina zote za unyanyasaji wa kijinsia na mazoea mabaya”


Polisi nchini humo tayari wamemkamata mume wa marehemu, akituhumiwa kumshambulia vikali na kusababisha kifo chake.


“UNFPA inaunga mkono mamlaka, jamii na wanaharakati wanaopinga ukatili wa kijinsia na wanaovunja haki za wanawake. Tunataka uchughuzi wa haraka ufanyike kuhusiana na mauaji, haya na vyombo vya usalama wahakikishe wanasimamia sheria za kuwalinda wanawake na watoto katika kutekeleza makubaliano ya ya kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake na mitakaba mingine ya kimataifa.”


Udhalilishaji wa kijinsia, ukatili majumbani, ni ukiukwaji wa haki za binadamu kwa wanawake na wasichana. Vitendo hivyo vya unyanyasaji vinaongeza na kuimarisha ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana na kuendeleza mzunguko mbaya ambao ni hatari kwa maendeleo yao na ufanisi.