Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waasi 22 wauawa huko Ituri, MONUSCO yadhibiti shambulio lao 

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa MONUSCO wakifanya doria katia eneo la Ituri ili kuzuia vitendo vya ADF.
MONUSCO
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa MONUSCO wakifanya doria katia eneo la Ituri ili kuzuia vitendo vya ADF.

Waasi 22 wauawa huko Ituri, MONUSCO yadhibiti shambulio lao 

Amani na Usalama

Takribani watu 30 wameuawa kufuatia shambulio la jumatatu huko Kinyanjojo na Boga kwenye jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. 

Radio Okapi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo , MONUSCO imesema kati ya hao waliouawa 22 ni washambuliaji waliokuwa wamejihami na 8 ni raia. 

MONUSCO kupitia mtandao wake wa Twitter inasema iliweza kudhibiti shambulio hilo na kukabiliana na wapiganaji katika tukio hilo lililofanyika kilometa 120 kusini mwa mji mkuu wa jimbo la Ituri, Bunia. 

Kwa mujibu wa taarifa hizo, operesheni zinaendelea kusaka washambuliaji waliokuwa wamejihami wakati huu ambapo wakazi wa maeneo ya Tchiabi na Boga, wanahofia mashambulizi ya visasi kutoka kwa waasi hao. 
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema, “washambuliaji walivamia maduka na kupora mali, jengo la hospitali kuu ya rufaa ya Boga lilinusurika kuteketea kwa moto.” 
Kwa mujibu wa radio Okapi, askari wa jeshi la serikali, FARDC alijeruhiwa huku maiti wanane raia walitambuliwa kwenye eneo hilo.