Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

António Guterres ameteuliwa tena na Baraza la Usalama kuongoza UN muhula wa pili 

Sven Jürgenson mwakilishi wa kudumu wa Estonia na Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi wa Juni akiendfesha mkutano wa kupendekeza uteuzi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
UN Photo/Eskinder Debebe)
Sven Jürgenson mwakilishi wa kudumu wa Estonia na Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi wa Juni akiendfesha mkutano wa kupendekeza uteuzi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

António Guterres ameteuliwa tena na Baraza la Usalama kuongoza UN muhula wa pili 

Masuala ya UM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limemchagua rasmi tena Katibu Mkuu wa sasa António Guterres kama mteule wake kutumikia muhula wa pili wa miaka mitano katika uongozi wa juu zaidi kwenye Umoja wa Mataifa.

Mapendekezo, yaliyotolewa katika azimio lililopitishwa na kwa kauli moja katika mkutano wa faragha, na sasa uteuzi huo unakwenda kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuidhinishwa rasmi na nchi wanachama 193.

Katika taarifa yake baada ya kuteuliwa tena Bwana Guterres amesema ni "heshima kubwa" kuchaguliwa, na akawashukuru mabalozi wanaohudumu katika Baraza la Usalama kwa kuweka imani yao kwake. "Shukrani zangu pia zinakwenda kwa Ureno, kwa kuniteua tena", ameongeza.

Ni heshima kubwa kwangu

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa "Imekuwa ni fursa kubwa kwangu kutoa huduma kwetu sis watu na kuongoza wanawake na wanaume wamakini wa Shirika hili kwa miaka minne na nusu iliyopita, wakati tumekuwa tukikabiliwa na changamoto nyingi ngumu na kubwa”.

Pia amesema kuwa akipata fursa nyingine “Nitakuwa mnyenyekevu sana endapo Baraza Kuu litaniamini na kunipa jukumu la muhula wa pili.”

Baraza la Usalama likikutana kujadili mapendekezo kwa ajili ya uteuzi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
UN Photo/Eskinder Debebe)
Baraza la Usalama likikutana kujadili mapendekezo kwa ajili ya uteuzi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Chini ya taratibu za kumteua mkuu mpya wa shirika hilo la kimataifa, baada ya pendekezo hilo kupitishwa kutoka Baraza la Usalama kwenda kwa Baraza Kuu, rasimu ya azimio inatolewa kwa ajili ya Baraza Kuu kuchukua hatua. 

Baada ya mashauriano yanayofaa na nchi wanachama, Rais wa Baraza Kuu hupanga tarehe ya rasimu hiyo kuchukuliwa hatua.

Taarifa ya maono yake

Mazungumzo yasiyo rasmi yalianzishwa wakati wa mchakato wa mwisho wa uteuzi katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na wazo la kuruhusu wagombea kutoa maoni yao na kuulizwa maswali kutoka kwa wawakilishi mbalimbali wa jamii ya kimataifa, pamoja na asasi za kiraia, ilikuwa ni mwanzo wa kiwango kipya cha uwazi .

Awamu sita za mwisho za kuchagua Makatibu Wakuu ziliteuliwa na Baraza Kuu kupitia azimio lililopitishwa kwa kauli moja.

Kura itafanyika tu ikiwa nchi mwanachama itaiomba na idadi kubwa ya wale wanaopiga kura itahitajika kwa Baraza kupitisha azimio hilo. 

Lakini Baraza linaweza kuamua kuwa uamuzi huo unahitaji wingi wa theluthi mbili wa kura kuamua.

Na ikiwa kura itapigwa, itakuwa ni kwa kura ya siri.

Mchakato wa kihistoria

Hati ya Umpoja wa Mataifa, iliyosainiwa mwaka 1945 kama msingi wa shirika, inaelezea kidogo juu ya jinsi Katibu Mkuu atakavyochaguliwa, kando na kifungu cha 97, ambacho kinabainisha kuwa mgombea "atateuliwa na Baraza Kuu baada ya mapendekezo ya Baraza la Usalama. ” Katika kikao chake cha kwanza mwaka 1946, Baraza Kuu lilikuwa likifanya kazi zaidi katika mchakato wa uteuzi.

Iiliunda azimio A / RES / 1/11 kuamua kwamba Baraza la Usalama litaongoza katika mchakato wa uteuzi, litakubaliana jina moja katika mkutano wa faragha, na kupitisha jina hilo kwenye Baraza Kuu kwa nnjia ya kura.