Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili zaidi unahitajika kwa ajili ya kusaidia watu wa Chad-OCHA 

Wakimbizi wa ndani Mellia, Chad
OCHA/Ivo Brandau
Wakimbizi wa ndani Mellia, Chad

Ufadhili zaidi unahitajika kwa ajili ya kusaidia watu wa Chad-OCHA 

Wahamiaji na Wakimbizi

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA leo imezindua mpango wa kukabiliana na  mahitaji ya kibinadamu kwa ajili ya Chad. 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi, msemaji wa OCHA Jens Laerke amesema Chad ambayo ina idadi ya watu milioni 17 kati ya hao milioni 5.5 wanahitaji msaada wa dharura. 

Kwa mujibu wa OCHA, Chad inakabiliwa na majanga aina tatu moja ni utapiamlo na ukosefu wa uhakika wa chakula na dharura ya kiafya na janga la wakimbizi kutokana na mzozo wa makundi yaliyojihami na majanga ya asili na haya yote yameongeza viwango vya mahitaji. 

Bwana Laerke amesema idadi ya wakimbizi waliolazimika kukimbia makwao kutokana na mazingira hatarishi imefikia watu milioni moja. Aidha watu milioni 4.6 hawana hukakika wa chakula na zaidi ya watoto milioni 4 chini ya umri wa miaka mitano na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha wanahitaji msaada wa lishe mwaka huu. Pia watu milioni 1.7 hawana huduma za afya za mara kwa mara. 

OCHA imesema mahitaji yanaongezeka huku ufadhili ukipungua. Mwak huu mashirika ya kibinadamu yanahitaji dola milioni 617 kwa ajili ya kusaidia watu milioni 4 na msaada wa chakula na lishe bora, huduma za afya, makazi, wáter, huduma ya kujisafi na usafi pamoja na huduma ya elimu kwa ajili ya watoto. 

Lakini kufikia nusu ya mwaka huu wa 2021, chini ya dola milioni 50 au asilimia 8 ya ombi limepatikana na ufadhili zaidi unahitajika haraka. 

Wakiwa na fedha na uwezo wa kufikia maeneo yote mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wanaweza kusaidia kuokoa maisha na hadhi ya mamilioni ya watu walioathirika Chad. Ufadhili utasaidia watu kuweza kuwajengea mnepo na kukabiliana na athari za siku zijazo na msaada utawalinda kutokana na ukiukwaji wa haki zao.