Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yatoa wito wa ushirikiano wa kimataifa kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kufikia SDGs

Mji Mkuu wa Jamhuri ya Kofrea , Seoul
Unsplash/Chinh Le Duc
Mji Mkuu wa Jamhuri ya Kofrea , Seoul

UN yatoa wito wa ushirikiano wa kimataifa kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kufikia SDGs

Tabianchi na mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akiongea leo katika mkutano muhimu wa ushirikiano wa kimataifa, amesema ikiwa serikali zitaafikiana kwa pamoja malengo ya kumaliza makaa ya mawe, kuongeza ahadi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kuwekeza katika malengo ya dunia, kuna fursa ya kuishinda "changamoto kubwa ya maisha yetu".

Katika ujumbe wake wa video kwenye mkutano ufunguzi wa mkutano wa mwaka 2021 wa P4G unaofanyika mjini Seoul Jamhuri ya Korea ameongeza kuwa dunia inahitaji ushirikiano wa kimataifa kushinda janga la coronavirus">COVID-19, kufikia Malengo ya maendeleo  ya maendeleo endelevu na kushughulikia mabadiliko ya tabianchi.

Mkutano huo wa ushirikiano wa ukuaji unaojali mazingira na malengo ya Ulimwengu 2030 (P4G) unakusudia kukuza ushirikiano wa soko na kuchagiza hatua za ngazi ya juu za kisiasa na sekta binafsi.

Na mkutano huo umewaleta pamoja wakuu wa nchi, wakurugenzi watendaji na viongozi wa asasi za kiraia karibu na ajenda ya pamoja ya kuhamasisha uwekezaji kwa ajili ya mabadiliko yanayoonekana.

Pengo la uzalishaji hewa ukaa

António Guterres ameelezea kwamba “ingawa kuna ahadi za kufanikisha kutozalisha kabisa hewa ukaa ifikapo 2050, bado kuna "mengi ya kufanya" ili kuziba pengo la uzalishaji wa hewa ukaa na kufikia malengo ya SDGs.”

Amesisitiza wito wake kwa wachaguzi wakuu wote kuwasilisha michango mipya waliyoamua Kitaifa, kujitolea kutozalisha kabisa hewa ukaa ifikapo mwaka 2050, na, 'muhimu zaidi', kuweka sera na mipango kuelekea kufikia lengo hilo.

"Kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi uso kwa uso kutasaidia kuwalinda watu walio katika mazingira magumu zaidi  wakati wa kujikwamu kutoka klwenye janga la COVID-19 “ amesema, akikumbusha kwamba kipaumbele cha kwanza sasa hivi ni kuweka mipango na sera kuzuia mitambo mipya ya makaa yam awe na kuacha matumizi ya makaa ya mawe ifikapo mwaka 2040.

Katika ujumbe huo, Katibu Mkuu amepongeza Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kutangaza kwamba itasimamisha fedha zote za kimataifa kwa ajili ya makaa ya mawe na kuhimiza mashirika mengine ya serikali na sekta binafsi kufanya vivyo hivyo.

 

Malengo ya maendeleo endelevu, SDGs
UN SDGs
Malengo ya maendeleo endelevu, SDGs

Mapengo ya fedha na mnepo

Bwana Guterres pia ameelezea wasiwasi wake juu ya pengo la fedha na mnepo wa kuhimili. 

Ameongeza kuwa “nchi zilizoendelea bado hazijatimiza ahadi ya kila mwaka ya dola bilioni 100 kwa juhudi za hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kusaidia jamii zilizo katika mazingira magumu ambazo tayari zinateseka na athari za ongezeko la joto duniani.”

Ameelezea pia kuwa mtu mmoja kati ya watatu ulimwenguni bado hawajafunika vya kutosha na mifumo ya tahadhari ya mapema, na wanawake na wasichana, ambao ndio asilimia 80 ya wale wanaolazimika kuhama kutokana na dharura ya mabadiliko ya tabianchi, bado mara nyingi hutengwa na maamuzi ya kushughulikia changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

"Tunahitaji haraka mafanikio katika kudhibiti hali na kujenga mnepo", ameongeza, akiuliza nchi zote za wafadhili kuongeza ahadi zao za kifedha.

Katika ujumbe wake, kwenye mkuu huo wa Umoja wa Mataifa ameangazia umuhimu wa kufadhili 'miundombinu ya kesho' kwa kusaidia nchi zinazoendelea kuelekea nishati endelevu na uchumi wa mzunguko huku zikizisaidia kupanua uchumi wao.

"Kwa kifupi, tunahitaji ushirikiano wa kimataifa kwa maendeleo ya kijani, na umoja, endelevu", amesisitiza.

Lengo la pamoja

Bwana Guterres ameonya kwamba “hakuna ushirikiano wa kimataifa ikiwa wengine wataachwa nyuma wakihaha kuishi" na akasema kuwa hii ni kweli kwa COVID na usambazaji wa chanjo na dharura ya mabadiliko ya tabianchi.

"Katika azma hii, Jamhuri ya Korea ni mshirika anayeongoza", amesema, akiipongeza serikali kwa ahadi yake ya 2050 ya kutozalisha kabisa hewa ukaa na mpango mpya wakulinda mazingira Korea.

Amesisitiza kuwa ikiwa serikali zitakubali malengo yale yale, kutakuwa na fursa ya ushirikiano wa kweli ambao utatuandaa "kuishinda changamoto kubwa ya maisha yetu".