Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres

Guterres anena na vijana walinda amani na kupongeza mchango wao.

UN News
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres

Guterres anena na vijana walinda amani na kupongeza mchango wao.

Amani na Usalama

Katika kuadhimisha siku ya walinda amani hii leo Katibu Mkuu Antonio Guterres amezungumza na vijana katika opefresheni za ulinzi wa amani upande wa polisi, jeshi na shughuli za kiraia  na kupongeza mchango wao katika amani na usalama.

Katika kuadhimisha siku ya walinda amani hii leo Katibu Mkuu Antonio Guterres amezungumza na vijana katika opefresheni za ulinzi wa amani upande wa polisi, jeshi na shughuli za kiraia  na kupongeza mchango wao katika amani na usalama. 

Katika mazun gumzo yao yaliyofanyika kwa njia ya mtandao wamegusia uwezo wa vijana katika kurejesha utulivu kwenye nchi zenye mizozo na umuhimu wao katika mchakato huo, athari za operesheni hizo na baadhi ya uzoefu watokako na waliko katika operesheni za ulinzi wa amani. 

Hivi sasa Umoja wa Mataifa una operesheni 12 zinazojumuisha Zaidi ya walinda amani 90,000 vijana kote duniani. 

Vijana ni chachu ya amani 

Kwa Katibu Mkuu , vijana sio tu kwamba wana mchango mkubwa katika kudumisha amani , lakini pia wana jukumu kubwa katika ujumuishwaji wa vijana katika mchakato wa amani kwenye nchi wanako hudumu. 

Kaulimbiu ya siku ya walindamani mwaka huu ni "Njia ya kuelekea amani ya kudumu:kukumbatia uwezo wa vijana kwa ajili ya amani na usalama". 

Katika mazungumzo yake na vijana hao ambao mwanajeshi, polisi na muhudumu raia wametiana moyo kwa kuzungumzia mambo yanayowachagija na kuwahamasisha lakini pia changamoto wanazokabiliana nazo. 

Polisi mkufunzi kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Mali , MINUSMA Sira Bojang anahudumu katika moja ya operesheni hatari zaidi za Umoja wa Mataifa duniani kwa sababu ya idadi kubwa ya vifo vya walindamani nchini humo. 

Kazi yake ni tathimini maeneo yalikofanyika uhalifu na katika mazungumzo na Katibu Mkuu amesema ana hamasa kubwa ya kusaidia wengine. 

Kwa sira kuwa mlindamani ni fura kubwa nay a kipekee ya kuona jinsi nchi zinavyofanya mambo tofauti. 

Amesema kuangalia jinsi gani watu wanavyoweza kuwa na fikra tofauti, lakini wanaweza kufanyakazi kwa pamoja kutimila lengo la pamoja.  

Umoja wa Mataifa umesema "Kwa miaka 72 zaidi ya walindamani milioni 1 wameshiriki katika operesheni mbalimbali za kijeshi na kiraia kuhudumu katika operesheni 71 za Umoja wa Mataifa. Kutoka nchi 125." 

Uzoefu wao 

Luteni Eric Manz amesema lengo lake ni kurejesha amani na kuzuia kile kilichotokea nchini mwake Rwanda kisitokee tena popote duniani. 

Ameelezea ugumu mkubwa katika historia uliowakabili raia wa Rwanda kwa sababu ya mauaji ya kimbari na anasema hiyo ndio sababu kubwa iliyomchagiza kujiunga na ulinzi wa amani. 

Meneja Carolina Meroni anasimamia kitengo cha taarifa na takwimu za ulinzi wa Watoto kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ujulikanao kama MONUSCO. 

MONUSCO ndio operesheni kubwa zaidi duniani ambako anaona fursa za vijana kuweza kufanyakazi. 

Mawazo mapya  

Bi. Carolina amessitiza kwamba vijana wanaoshiriki ulinzi wa amani wanaweza kuleta mawazo mapya ya kushughulikia changamoto na matatizo ya muda mrefu. 

Kwake yeye changamoto ni kwa kundi hilo kusikilizwa na kushirikishwa katika mchakato wa kufanya maamuzi na kuketi katika meza ya majadiliano. 

Meroni amewachagiza vijana kote duniani kushikamana kufanyakazi kwa ajili ya kuwa na ulimwengu bora.