Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Niko hai, lakini nahisi nimekufa:Mhamiaji aliyenusurika kifo na Kapoteza watoto 3 baharini 

Misrah amepoteza watoto wake watatu walikufa maji wakati boti waliyokuwa wakisafiria kuzama kwenye Ghuba ya Aden
© IOM 2021/Hawa Diallo
Misrah amepoteza watoto wake watatu walikufa maji wakati boti waliyokuwa wakisafiria kuzama kwenye Ghuba ya Aden

Niko hai, lakini nahisi nimekufa:Mhamiaji aliyenusurika kifo na Kapoteza watoto 3 baharini 

Amani na Usalama

"Nimepoteza kila kitu," anasema Misrah, mwanamke mhamiaji akijitahidi kusimulia tukio la kutisha mno  la kushuhudia vifo vya watoto wake watatu baharini 

Misrah ni mwwanamke kutoka Ethiopia mwenye umri wa miaka 27, yeye pamoja na mumewe na watoto wake, Aziza mwenye umri wa miaka mitano; Rachar wa miaka mitatu; na Ikram wa miaka miwili, na wahamiaji wengine 55 na wakimbizi walikuwa ndani ya mashua iliyomilikiwa na wasafirishaji waliokuwa wakivuka Ghuba ya Aden kuingiacYemen kutoka Pembe ya Afrika kupitia Djibouti,  mnamo tarehe 12 Aprili mwaka huu wa 2021. 

Kwa sababu mashua ilikuwa imejaa pomoni lakini pia sababu ya kusafiri usiku wa manane, chombo kilipinduka kutokana na uzito wa kupindukia wa abiria.  

Watoto kumi na sita wakiwemo wa Misrah na angalau wahamiaji wengine 44 na wakimbizi walizama, wakiwa wamenaswa chini ya chombo hicho 

Yeye na mumewe Abdul Basit walikuwa ni miongoni mwa watu 14 tu walionusurika katika ajali hiyo. 

Akizungumza kupitia mtafsiri, Misrah anajipa nguvu na ujasiri kuelezea nyakati kabla ya msiba kufikwa na msiba huo mkubwa. 

"Tulipokuwa tunakaribia pwani ya Djibouti, mashua ilianza kupinduka," anakumbuka. “Watoto wangu walikuwa wamelala wakati mashua ilipinduka. Nilikuwa nimemshika Ikram mikononi mwangu. Nilijua ninaweza kuogelea. Ndivyo nilivyonusurika. Kwa bahati mbaya, watoto hawakunusurika. Walikuwa wadogo sana; mawimbi ya bahari yaliwazidim nguvu.” 

Wahamiaji ambao walinusurika kwenye boti ya wasafirishaji haramu kwenye ghuba ya Aden walifikishwa ufukweni Obock Djibout
© IOM/Olivia Headon
Wahamiaji ambao walinusurika kwenye boti ya wasafirishaji haramu kwenye ghuba ya Aden walifikishwa ufukweni Obock Djibout

Pekee yake, Misrah aliogelea hadi ufukweni, akienda kwa miguu na kwa msaada wa mwendesha magari aliyekuwa anapita kwenda mji wa Obock, Djibouti, aliweza kufika na kutana na wafanyikazi kutoka kituo cha kukabiliana na masuala ya uhamiaji cha Shirika la Umoja wa mataifa la Uhamiaji (IOM). 

“Nilipewa simu kumpigia mama yangu na ninajisikia vizuri kwa sasa. Baadaye pia walisaidia kumpata mume wangu, ambaye alirudi Ethiopia, ”Misrah anasema. 

“Wafanyakazi wananijali, wakijaribu kunihakikishia usalama wang una ningependa kumuona mama yangu kwani ndiye pekee anayeweza kunifariji sasa hivi .” ameongeza kusema mama huyo mwenye machungu makubwa. 

Mwaka 2012, Misrah aliondoka nyumbani kwake huko Derdawah, Ethiopia, kwenda kutafuta kazi. 

"Nilitaka kutunza familia yangu, mama yangu na ndugu zangu," anaelezea. “Nilifanikiwa kusafiri kwenda Djibouti ambako nilifanya kazi ya kijakazi. Pesa niliyopata kupitia hiyo kazi ilikuwa ndio nauli ya kusafiri kwenda Yemen kwa mashua. ” 

Maelfu ya wahamiaji kutoka Ethiopia hupitia Djibouti kwenda Yemen kila mwaka wakitarajia kufika Ufalme wa Saudi Arabia, ambapo kuna fursa nzuri zaidi za kazi na kipato cha juu kuliko nyumbani. Wengine kama Misrah wanakusudia kubaki Yemen ambapo, kabla ya mzozo na janga la sasa, kulikuwa na fursa kwa wafanyikazi wahamiaji.  

Kihistoria, kumekuwa na msafara kila wakati kati ya Yemen na Pembe ya Afrika. 

Polepole, Misrah alijenga maisha mapya katika jiji la Aden, kwa kazi ya usafishaji. Mwaka 2014 aliolewa na Abdul Basit, na wakaanzisha familia yao. 

"Nilipenda maisha yangu nchini Yemen," Misrah anasema. 

Wafanyakazi katika kituo cha wahamiaji cha IOM mjini Obock Djibout wakitoa msaada kwa wahamiaji wanaotaka kurejea nyumbani
© IOM 2020/Alexander Bee
Wafanyakazi katika kituo cha wahamiaji cha IOM mjini Obock Djibout wakitoa msaada kwa wahamiaji wanaotaka kurejea nyumbani

Wakati mama mzazi wa Misrah aliugua tena nchini Ethiopia, alihisi kulazimika kurudi ili amtunze. Mumewe alikuwa na wasiwasi juu ya usalama wa Misrah, na mwishowe, waliamua kusafiri pamoja kama familia; hakututaka Misrah asafiri pekee yake.  

Kama wahamiaji wengi wasio na hati katika eneo hilo, hawakuwa na hati rasmi za kukaa nchini Yemen au karatasi zilizohitajika kurudi nchini Ethiopia, na walilazimika kuwalipa wasafirishaji haramu dola 400 ili wasafiri kutoka Yemen kwenda Djibouti kwa mashua, awamu ya kwanza ya safari kwenda Ethiopia. Mara nyingi, safari hii inaweza kugharimu zaidi. 

Katika mwaka uliopita, zaidi ya safari 11,000 kama hizo zilifanywa kutumia vyombo vya bahari visivyofaa na wahamiaji kutoka Pembe ya Afrika wakiwa na hamu ya kurudi nyumbani kutoka Yemen.  

Wengine, kama Misrah, wanarudi kwa dharura za kifamilia, wakati wengine walikuwa wamejaribu na wakashindwa kufika Ufalme wa Saudi Arabia.  

Janga la COVID-19 limesababisha vizuizi vya harakati za safari kote Pembe ya Afrika na nchini Yemen, pamoja na usalama ulioimarishwa katika mpaka wa Yemen na Ufalme wa Saudi Arabia.  

IOM inakadiria kuwa zaidi ya wahamiaji 32,000 wamekwama nchini Yemen. 

Hali mbaya ambayo wahamiaji milioni 2.7 waliokwama kutokana na janga la COVID-19 wanapitia, ni pamoja na kukamatwa na kuwekwa kizuizini, kutekwa nyara, kuteswa, unyanyapaa na unyanyasaji mwingine, iligunduliwa katika ripoti ya kimataifa ya IOM  ya kikosi kazi cha shirika hilo kinachohusika na wahamiaji wanaorejea iliyotolewa Oktoba 2020. 

Wahamiaji toka Ethiopia wakivuja jangwa la Djibouti
© IOM 2020/Alexander Bee
Wahamiaji toka Ethiopia wakivuja jangwa la Djibouti

Wafanyikazi wa IOM nchini Djibouti wanampa Misrah ushauri kutokana na  kiwewe alichokipata lakini pia msaada mwingine, na kufanya kazi na IOM nchini Ethiopia ili kumsaidia kurudi nyumbani aweze kuungana tena na mumewe na mama yake. 

“Kabla sijaondoka Djibouti, ninataka kuwaaga watoto wangu. Ningependa kupata fursa ya kuwaomboleza kwenye kaburi kabla ya kurudi Ethiopia, ” anasema Misrah 

Ataendelea kupata ushauri nasaha kutoka IOM Ethiopia na, pamoja na mumewe Abdul Basit, watasaidiwa kurudi katika jamii yao na kuanza kujenga tena maisha yao.  

Lakini Misrah anasema huzuni ya kuwapoteza watoto wake watatu, Aziza, Rachar na Ikram, haitaondoka kamwe moyoni mwake. 

 "Ninataka wahamiaji nchini Yemen waelewe kwamba safari hiyo ni hatari sana," anasema. "Niko hai, lakini nahisi kama nimekufa." 

Cha kusikitisha ni kwamba zaidi jumla ya wahamiaji 100 sasa wamekufa  maji kupitia visa kama hivyo katika pwani ya Djibouti kwa miezi sita iliyopita.  

Hivi mwezi jana tu, wahamiaji 80 waliokuwa wakisafiri kutoka Djibouti kwenda Yemen walitelekezwa na mashua na wasafirishaji haramu na kadhaa walifariki dunia.  

Mwisho wa mwaka jana, wahamiaji wasiopungua 50 walikufa katika misiba sawa na hiyo. 

IOM inafanya kazi kuwasaidia wahamiaji waliokwama kufika nyumbani salama. Serikali ya Ethiopia imethibitisha utaifa wa wahamiaji 1,100 wasio na hati, na ndege mbili za kwanza za hiari za kibinadamu zilitoka mwezi Machi na Aprili.  

Wahamiaji waliobaki watarudi katika wiki na miezi ijayo. Mjini Aden pekee, IOM imesajili zaidi ya watu 6,000 ambao wanataka msaada wa kurudi nyumbani na maelfu zaidi kote Yemen pia watapata msaada. 

Wahamiaji kutoka Ethiopia wakiwa kwenye pwani ya Obock, Djibout
© IOM 2020/Alexander Bee
Wahamiaji kutoka Ethiopia wakiwa kwenye pwani ya Obock, Djibout

 Licha ya hadithi kama za Misrah na hatari dhahiri za kutishia maisha za safari za baharini, idadi ya wahamiaji wanaofika Djibouti kwa mashua inaendelea kuongezeka. Mnamo mwezi Machi, zaidi ya wahamiaji 2,343 waliwasili kutoka Yemen kwa mashua, ikilinganishwa na 1,900 kwa mwezi wa Februari. 

IOM inafanya kazi na serikali na washirika wengine kukidhi mahitaji ya wahamiaji hawa, kupunguza uhamiaji usio wa kawaida, na kuwalinda wahamiaji dhidi ya unyonyaji unaofanywa na wasafirishaji haramu na wauzaji wa binadamu.