Masomo shuleni na vyuoni yaendane na hali halisi kwenye jamii – Benki Ya Dunia Ghana

27 Mei 2021

Nchini Ghana Benki ya dunia pamoja na vijana wamebaini kuwa kwa kiasi kikubwa masomo yanayofundishwa shuleni na vyuoni hayamwezeshi kijana kujikimu na maisha pindi anapohitimu masomo na mara nyingi vijana kujikuta wakifanya shughuli ambazo hata hawakuzisomea.

Huyo ni mmoja wa vijana wa nchini Ghana ambaye aliulizwa kama ujuzi anaoutumia katika shughuli zake za kujipatia kipato, aliupata shuleni. Anasema, sikuupata ujuzi huu shuleni. 

Hali hiyo ndio inayowakumba vijana wengine nchini humo, ambao wamejikuta baada ya masomo wakirejea kuishi maisha yale yale sawa na wenzao ambao hawakuendelea na masomo. Mathalani msichana huyu…. anasema aliishia darasa la 6, anafanya shughuli ndogondogo za mtaani, huyu mwingine anasema…. aliishia elimu ya kati, sasa ni mvuvi, na huyu mwingine…. anasema yeye ana shahada ya chuo kikuu amesomea masuala ya benki na fedha lakini sasa anafanya kazi ya kutengeneza vitatu. Tatizo ni nini hasa? Mawuko Fumey ni afisa wa Benki ya Dunia nchini gani anayehusika na ulinzi wa jamii na kazi anasema, “Tuligundua kwamba mfumo wa sasa umewekwa kwa namna ya fanya mtihani na faulu, hali ambayo haisaidii mtu kuweza kuendana na soko la ajira.» 

Chapisho la Ajira kwa Vijana la Benki ya Dunia nchini Ghana linasema maeneo ya kipaumbele kwa ajira kwa vijana katika maeneo ya vijijini na mijini, ni kilimo na kilimo cha biashara, mafunzo ya ujuzi, kukuza ujasiriamali na maeneo mengine kama hayo yenye faida kubwa. 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter