Tukiukumbuka mchango wa Budha tujenge maisha ya amani na utu kwa wote:Guterres 

26 Mei 2021

Leo ni siku ya kimataifa ya Vesak ambayo ni siku takatifu kwa watu wa dini ya Kibudha siku ambayo inaenzi na kutamini mchango wa dini hiyo katika utamadfuni na Imani. 

Katika ujumbe wake maalum wa siku hii ambayo huadhimishwa kila mwaka Mei katika majira ya chipukizi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mwaka huu maadhimisho yanafanyika dunia ikiwa bado inapambana na janga la corona au COVID-19 ni muhimu kuendelea msingi wa siku hii. 

“Ujumbe huu wa umoja na huduma kwa wengine usiopitwa na wakati ni muhimu zaidi sasa kuliko wakati mwingine wowote. Ni kwa pamoja tu ndio tutaweza kukomesha kusambaa kwa maambukizi ya corona na kujikwamua vyema na janga hili.” 

Guterres ametuma salamu kwa waumini wote wa Kibudha duniani katika kuadhimisha siku hii huku wakienzi kuzaliwa, kupewa upako na kufa kwa mkuu wa Budha. 

Ameongeza kuwa “Leo tunatambua mchango wa dini ya Kibudha kwa imani ya binadamu na utamaduni kwa zaidi ya milenia mbili na nusu. Sote mabudha na wasio Mabudha tunaweza kuchagizwa na ujumbe wa Kibudha wa ukweli, wa huruma na unaoheshimu viumbe vyote. Wakati tunakabiliwa na athari za muda mrefu za COVID-19, ni dhahiri sasa kuliko wakati mwingine wowote kwamba ubinadamu na utu ni vitu vya muhimu kwa ustawi wetu na wa sayari yetu.” 

"Vesak", Siku ya mwezi uliokamili na huadhimishwa mwezi wa Mei. Ni siku takatifu zaidi kwa mamilioni ya Wabudha ulimwenguni kote.  

Na ilikuwa siku ya Vesak milenia mbili na nusu zilizopita, mwaka wa 623 Kabla ya Kristo (KK), ambapo Buddha alizaliwa.  

Ilikuwa pia ni katika siku ya Vesak ambapo Budha alipata upako, na ilikuwa ni siku ya Vesak a,mbaypo Budha katika mwaka wake wa 80 alikufa. 

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha , azimio lake namba 54/115 la mwaka 1999, lililoitambua kimataifa siku ya Vesak kwa kutambua mchango ambao Ubudha, mojawapo ya dini za zamani zaidi ulimwenguni, umetoa kwa zaidi ya milenia mbili na nusu na unaendelea kutoa kwa ubinadamu wa kiroho . 

Siku hii inaadhimishwa kila mwaka katika Makao Makuu ya Umoja wa Matyaifa na ofisi zingine za Umoja wa Mataifa, kwa kushirikiana na ofisi za balozi za kudumu za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na misioni ya kudumu. 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter