WFP yaimarisha msaada kwa maeneo yaliyohatarini kukumbwa na njaa 

24 Mei 2021

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP limeimarisha msaada wa chakula katika maeneo yanayokabiliwa na njaa nchini Yemen kama sehemu ya kuzuia baa la njaa lakini uwezo wa shirika hilo kuendelea na shughuli hadi mwishoni mwa mwaka ziko njia panda. 

Mkurugenzi wa WFP nchini Yemen Laurent Bukera amesema, “udhaifu wa Yemen ukijumuishwa na vichocheo vya uhakika wa chakula umeacha Yemen katika hatari ya viwango vya juu vya njaa na mazingira ya njaa. Ameongeza kwamba, ongezeko la machafuko, kudorora kwa uchumi, kupand akwa bei ya bidhaa na janga la COVID-19 vimechangia katika ongezeko la njaa kwa mwaka uliopita." 

Takriban watu 50,000 nchini Yemen wanaishi katika mazingira ya njaa na watu milioni 5 wako katika hatari. Mtu mmoja anafariki dunia katika kila dakika kumi kutokana na magonjwa yanayozulika kwa mfano kuhara, utapiamlo na mambukizi ya mfumo wa kupumua. 

WFP imerejelea kuwasilisha mahitaji ya dharura mwezi uliopita baada ya kupokea ufadhili na inafikia watu milioni sita katika majimbo tisa yaliyohatarini ikiwemo Hajjah, Al Jawf, Amran, Al Hodeidah, Raymah, Al Mahwit, Sa’ada, Dhamar na Taiz. 

Kuanzia mwezi Juni watu hawa watapokea mlo wa siku kamili kila mwezi  

Njaa imeongezeka nchini Yemen wakati mzozo ukiendelea kuongezeka, na kufurusha familia kwa mara ya tatu au nne wakati vita vikiendelea kwa mwaka was aba. 

Ongezeko la bei ya vyakula kwa asilimia hadi 200 zaidi ya viwango vya kabla ya vita na imefanya mamilioni ya watu kushindwa kununua chakula. Isitoshe awamu ya pili ya  janga la COVID-19 limepiga maeneo mengi Yemen na mfumo wa afya unashindwa kumudu. 

 Kama azimio la Baraza la Usalama la Usalama namba 2417 lililopitishwa miaka mitatu iliyopita mwezi Mei linavyosema mnyororo wa njaa na mzozo unamanisha aman ndio suluhu pekee kwa mzozo wa njaa nchini Yemen. Hadi siku hiyo, msaada wa kibinadamu ni muhimu na upungufu wa ufadhili unaweza kuwa na madhara mabaya kwa wayemeni. 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter