Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Kimataifa ya bionuai inataka kuamsha hatua ya kila mtu: Guterres 

Jua likiwa linatuama katika hifadhi ya taifa ya Acadia, Maine.
UN News/Elizabeth Scaffidi
Jua likiwa linatuama katika hifadhi ya taifa ya Acadia, Maine.

Siku ya Kimataifa ya bionuai inataka kuamsha hatua ya kila mtu: Guterres 

Tabianchi na mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, katika ujumbe, wake kuhusu siku ya kimataifa ya bionuai inayoadhimishwa kila tarehe 22 mwezi Mei, amekumbushia kwamba idadi ya aina fulani za wanyama na mimea inapungua kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea; janga linaongeza hatari ya magonjwa yanayosambazwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa wanadamu kama vile Covid-19. 

Kaulimbiu ya mwaka huu kuhusu siku hii ni "sisi ni sehemu ya suluhisho" na inakumbusha kwamba bionuai inabaki kuwa jibu kwa changamoto kadhaa za maendeleo endelevu. 

Bwana Guterres amesema, "bionuai inapungua kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea na cha kutisha na mashinikizo yanaongezeka." 

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, raslimali zinapungua haraka kuliko asili inavyoweza kuzijaza tena.” 

Aidha Bwana Guterres amesema, "janga la virusi vya corona, “limetukumbusha uhusiano wa karibu kati ya watu na maumbile" na kwamba sasa kuna fursa ya kupona vizuri. 

Guterres amesema ni muhimu kulinda asili, kurejesha mazingira na kuweka usawa katika uhusiano na sayari. Ikiwa hiyo itatokea, anasema kwamba "faida zitakuwa kubwa." 

“Kwa kurejesha bioanuwai iliyopotea, itawezekana kuboresha afya ya binadamu, kufikia maendeleo endelevu na kukabili dharura ya tabianchi.” Ameshauri Bwana Guterres.