Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UN akaribisha sitisho la mapigano Gaza

Kiwango cha uharibifu huko Ukanda wa Gaza.
UNOCHA/Samar Elouf
Kiwango cha uharibifu huko Ukanda wa Gaza.

Katibu Mkuu wa UN akaribisha sitisho la mapigano Gaza

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa -UN, Antonio Guterres amekaribisha kusitishwa kwa mapigano kati ya Gaza  na Israel huko Mashariki ya Kati, mapigano ambayo  yamedumu kwa siku 11.

Msemaji wa UN Stephane Dujarric katika taarifa aliyoitoa leo jijini New York Marekani kwa vyombo vya habari ,amesema katibu mkuu ametuma salamu za pole kwa waathirika wa mapigano “Natuma rambirambi zangu kwa waathirika na mapigano na wapendwa wao”

Taarifa ya Dujarric inasema, katibu Mkuu Guterres amewapongeza waliosaidia mazungumzo ya kusitishwa kwa mapigano akisema, “naipongeza Misri na Qatar kwa mchango wao kwa kushirikiana na Umoja wa mataifa katika kuleta suluhu na kurejesha amani baina ya Palestina na Israel. Nahimiza pande zote kuendeleza makubaliano ya kusitisha mapigano”

Tweet URL

Wito pia umetolewa kwa jumuiya za kimataifa kusaidia wapalestina katika kujenga taasisi zao zilizoathirwa vibaya na mapigano, huku akihimiza Israel na Palestina kurudi kwenye meza ya mazungumzo.

“Nasisitiza, viongozi wa Israel na Palestina wana jukumu la kurudisha utulivu na kuanza mazungumzo ya kina kujadili kiini cha mzozo. Ukanda wa Gaza ni sehemu muhimu kwa paadae kwa taifa la Palestina na hakuna juhudi yeyote inayopaswa kuachwa kama kweli tunataka kufikia maridhiano ambayo yatamaliza mgawanyiko “

Taarifa inaeleza kuwa Guterres ametilia mkazo utayari wa Umoja wa Mataifa kukaa chini na Israel na palestina pamoja na wadau wP kimataifa na kikanda ikiwemo ukanda wa Mashariki yaKati  kurudi katika   mazungumzo yenye tija ya kutafuta suluhu ili kmaliza mzozo  huku akihimiza kurejelea makubaliano ya mwaka 1967 ya kuruhusu eneo hilo kukaliwa na nchi mbili kwa amani.

 Kuhusu nini kitatokea baada ya kusitishwa kwa mapigano

 Katibu Mkuu Guterres amesisitiza kuelekeza nguvu kuwasaidia walioathirika na machafuko na kujikita kupata suluhu ya kweli akisema, “nafikiri tutatakiwa kwanza kuimarisha usitishwaji wa mapigano, nadhani itakuwa muhimu kuwa na mpango thabiti wa kutoa misaada ya kibinadamu na kusaidia kupona kwa Gaza. Na nadhani itakuwa muhimu sana kufufua mchakato wa amani, mchakato wa suluhu ya kuwa na nchi mbili."