Programu ya rafiki imenipa ujasiri niliohitaji kuanza maisha mapya Ubelgiji:Mkimbizi Marie-Reine

18 Mei 2021

Kutana na mkimbizi Marie-Reine kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, ambaye sasa amepata hifadhi na anaishi Namur nchini Ubeligiji. Alipowasili hakujua yeyote na wala wapi pa kuanzia ili kuweza kujikimu katika nchi ya tatu ugenini, lakini kupitia program ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ijulikanayo kama “Rafiki” ambayo ni ya muongozo wa kukuza stadi na ujuzi ili kuwasaidia wakimbizi na waomba hifadhi, Marie-Reine amefungua ukurasa mpya wa maisha yake.

Mjini Namur Ubelgiji Marie-Reine akiwa na rafiki mpya Stéphane, ambaye ni meneja wa Benki. 

Marie ni mtu wa haya sana na anasema…..mara ya kwanza walipokutana na Stephane alishindwa hata kumtazama usoni. 

Stephane ambaye amekuwa akisaidia wakimbizi na waomba hifadhi kwa muda sasa kupitia program hiyo amedhamiria kumsaidia Marie-Reine kupata kazi,“Nadhani aliogopa ntamuuliza maswali mengi, hivyo nikafikiria ntazungumza naye tu kuhusu kazi yangu kwanza na kile ninachoweza kumsaidia”. 

Marie-Reine na Stéphane walikutana kwenye program ya UNHCR ya Rafiki ambayo inayotoa muongozo wa kukuza stadi na ujuzi kwa wakimbizi na waomba hifadhi. Merie-Reine anasema,“Nilipokuwa mtoto nilidhani ntakuwa na maisha mazuri mbele yangu. Lakini vita vilizuka na nilipowasili hapa nilikuwa peke yangu na ilikuwa vigumu sana, mwanzoni nilikuwa nalia kila usiku.  

Hata hivyo kupitia program ya Rafiki Marie-Reine sasa anajiamini,“Stéphane amenisaidia sana, amenifunza jinsi ya kuonekana na kujieleza mbele ya mwajiri, pia kubadili mapungufu na udhaifu wangu kuwa sifa zinazohitajika.” 

Mara mbili kwa mwezi Marie-Reine na Stephane wanakutana na kufanyiakazi vitu kama kuandaa wasifu wa kitaaluma wa Marie  na kutayarisha barua za maombi ya kazi. 

Kwa msaada wa Stephane sasa soni ya Marie-Reine imetoka , lakini si hilo tu amefanikiwa kupata ajira ya mafunzo kwa vitendo jambo ambalo Marie-Reine anasema limempa matumaini mapya na anajivunia sana. 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter