Maendeleo ya Tehama yasimuache mtu nyuma: Antonio Guterres

17 Mei 2021

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya mawasiliano na habari kwa jamii, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma ujumbe wa kuhimiza kuwajumuisha watu wote katika maendeleo ya tehama.

Guterres amesema maendeleo ya tehama yamesaidia Maisha ya watu kwenye afya na mafunzo kwa mabilioni ya watu. Katika janga la Corona au Covid-19 biashara, serikali na jamii ya kidijitali zimethibitisha ujasiri wao na ubunifu, na pia kusaidia kulinda watu na maisha yao.

Kipindi hiki cha wakati mgumu wa janga la Corona kimesaidia kuleta mabadiliko ya haraka kila sehemu. Lakini pamoja na mabadiliko hayo watu Bilioni 3.7 ambao ni takribani nusu ya watu wote duniani hawajaunganisha mtandaoni, watu hawa wengi wao ni wanawake.  Watu hawa ni lazimwa nao waunganishwe kama tuna dhamira ya kufikia maendeleo ya 5G, Ufahamu wa bandia, kufikisha matumizi ya tehama kwenye kila kitu ikiwemo afya na maendeleo mengine yenye kuleta mabadiliko endelevu.

Ameongeza kuwa nilazima kujilinda dhidi ya hatari zinazoletwa na maendeleo ya kiteknolijia, kuanzia kuenezwa kwa habari za chuki, habari za upotoshaji mpaka kushambuliwa mitandaoni na pia kuzuia matumizi mabaya ya taarifa za wanaotumia mitandao.

Umoja wa Mataifa kupitia Dira yake ya ushirikiano wa kidigitali na ufanyaji kazi na Muungano wa Mawasiliano duniani -ITU unadhamiria kuleta madiliko ya usawa, usalama, kuwajumuisha wote na unafuu, yote haya yatafanyika huku kukiwa na uheshimu wa haki za binadamu

Katika siku hii ya kimataifa ya Mawasiliano na Habari kwa jamii amehimiza jamii kwa ujumla kuazimia kufanya kazi kwa pamoja kutokomeza corona na kuhakikisha maendeleo ya teknolojia yanakuwa chanya yenye kusaidia kutimiza malengo ya maendeleo endelevu na kutomuacha mtu yeyote nyuma ya maendeleo haya.

 

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter