Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia zaendelea Yerusalem Mashariki, UN yapaza sauti 

Polisi wakiwa mtaani Sheikh Jarrah mashariki mwa Yerusalem ambako wapalestina wanatishiwa kufurushwa.
Yahya Arouri
Polisi wakiwa mtaani Sheikh Jarrah mashariki mwa Yerusalem ambako wapalestina wanatishiwa kufurushwa.

Ghasia zaendelea Yerusalem Mashariki, UN yapaza sauti 

Haki za binadamu

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa Michelle Bachelet ameelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na muendelezo wa ghasia katika maeneo yanayokaliwa ya wapalestina ikiwemo Yerusalemu mashariki na Israel katika siku za hivi karibuni. 

Msemaji wa Bachelet, Rupert Colville akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini Geneva Uswisi, amesema machafuko yanayoendelea ni ukiukwaji wa haki za binadamu akinukuu takwimu  kuhusu majeruhi na vifo. “Kwa mujibu wa Shirika la wapalestina la  Hilal nyekundu, wapalestina 915 wamejeruhiwa kati ya tarehe 7 na 10 ya mwezi huu wa mei huko Yerusalemu mashariki na zaidi ya 200 huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kutokana na mashambulizi kutoka vikosi vya usalama vya Israel.  Mpalestina mmoja mwenye uraia wa Israel ameripotiwa kuuwawa nchini Israel. Mpaka kufikia jana mei kumi askari 20 wa Israel wamejeruhiwa kutokana na machafuko hayo.” 

Bwana Colville ameviasa vyombo vya usalama vya vya Isarel kuhakikisha vinalinda haki za binadamu na uhuru wa kijieleza na kukusanyika akisema, “ Hakuna haja ya kutumia nguvu kwa wale wanaotekeleza haki yao ya kujieleza na kukusanyika,na iwapo kutakuwa na uhitaji wa kutumia nguvu basi itatakiwa kufuata muongozo wa kimataifa wa haki za binadamu. Tuna wasiwasi Zaidi na athari zinazowapata watoto na tunatoa wito kwa UNICEF kuhakikisha watoto wanalindwa na kuondolewa kwenye hatari ya kupata madhara.” 

Rupert Colville pia ametoa wito kwa wa watoto waliokamatwa kutokana na ghasia zinazoendelea waachiliwe huru.