Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za kujikwamua na COVID-19 zakumbana na kigingi, huku wagonjwa wakiongezeka:WESP 

Usafirishaji wa bidha kwa kutumia mkokoteni, Lima Peru.
IMF/Ernesto Benavides
Usafirishaji wa bidha kwa kutumia mkokoteni, Lima Peru.

Juhudi za kujikwamua na COVID-19 zakumbana na kigingi, huku wagonjwa wakiongezeka:WESP 

Afya

Juhudi za kimataifa za kujikwamua kiuchumi na janga la corona au COVID-19 ziko katika tishio kubwa, huku idadi ya wagonjwa ikiendelea kuongezeka na utoaji wa chano katika nchi masikini ukidemadema na pengo la usawa likitumbukiza nyongo matarajio ya ukuaji wa uchumi kwa silimia 5.4 mwaka huu wa 2021 kwa mujibu wa ripoti ya hali na matarahjio ya uchumi duniani (WESP). 

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa ya takwimu za nusu ya mwaka huu iliyotolewa leo inasema wakati mtazamo wa ukuaji wa uchumi kote duniani umeimarika ukiongozwa na Uchina na Marekani,lakjini ongezeko la maambukizi ya COVID-19 na hatua ndogo zilizopigwa kwa upande wa chanjo katika nchi nyingi vinatishia wigo mpana wa kujikwamua na janga hilo kiuchumi . 

Ripoti hiyo ambayo imeandaliwa na idara ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa DESA imeongeza kuwa kufuatia kusinyaa kwa uchumi kwa asilimia 3.6 mwaka 2020, uchumi wa dunia hivi sasa unatarajiwa kupanuka kwa asilimia 5.4 mwaka 2021, ukionyesha marekebisho ya juu kutoka kwa utabiri wa Umoja wa Mataifa uliotolewa mwezi Januari.  

Katikati Wakati kukiwa nah atua za haraka za chanjo na kuendelea kwa hatua za  misaada ya kifedha, China na Merika nchi mbili zenye uchumi mkubwa duniani ziko kwenye njia muafaka ya kujikwamua. 

Kinyume na hali hiyo mtazamo wa ukuaji wa uchumi katika nchi kadhaa za Asia Kusini, Agfrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, na Amerika Kusini na Caribbea zinasalia katika hali tete ya sintofahamu. 

Kwa nchi nyingi, ripoti inasema pato la uchumi linatarariwa krejea kwenye viwango vya kabla ya kuzuka kwa gonjwaifikapo mwaka 2022 au 2023. 

Mchuuzi wa mayai akiwa Quiapo nchini Ufilipino.
IMF/Lisa Marie David
Mchuuzi wa mayai akiwa Quiapo nchini Ufilipino.

Kujikwamua imara lakini kusiko linganifu 

Mchumi mkuu wa Umoja wa Mastaifa Elliott Harris katika ripoti hiyo amesema "Ukosefu wa usawa wa chanjo kati ya nchi na kanda unaleta hatari kubwa kwa jitihaza za kujikwamua pamoja na janga hilo ambazo tayari zinakabiliwa na kutokuwepo na usawa duniani. Ufikiaji wa chanjo ya COVID-19 kwa wakati unaofaa na kwa wakati wote itamaanisha tofauti kati ya kumaliza janga mara moja na kuweka uchumi wa ulimwengu kwenye njia ya kujikwamua tena, au kupoteza miaka mingi zaidi ya ukuaji, maendeleo na fursa." 

Kwa mujibu wa ripoti kujikwamua kwa uimara lakini kunakotofautiana katika biashara ya kimataifa na biashara ya bidhaa tayari kumezidi viwango vya kabla ya kuzuka kwa janga, kukichangiwa na mahitaji makubwa ya vifaa vya umeme na kielektroniki, vifaa binafsi vya kujinga na bidhaa zingine zilizotengenezwa. 

Ripoti imeendelea kusema “Uchumi unaotegemewa na utengenezaji wa bidhaa umekuwa mzuri, wakati wa shida na kipindi cha kujikwamua, lakini changamoto ya kutojikwamua haraka inasalia katika uchumi unaotegemea utalii na uzalishaji wa bidhaa.” 

Pia imeongeza kuwa biashara katika huduma, haswa utalii, itabaki kuwa na unyogovu wakati wa kuondoa polepole vizuizi katika safari za kimataifa na hofu ya milipuko mipya ya maambukizo katika nchi nyingi zinazoendelea. 

Mwanamke akitengeneza barakoa za kuuza wakati huu wa janga la COVID-19 akiwa Johannesburg Afrika Kusini.
IMF Photo/James Oatway
Mwanamke akitengeneza barakoa za kuuza wakati huu wa janga la COVID-19 akiwa Johannesburg Afrika Kusini.

Wanawake wameathiriwa vibaya zaidi na janga hilo 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo “wanawake wameathiriwa vibaya zaidi na janga la COVID-19 na Wanawake ndio wamekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya janga hilo. Pia wameathirika kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kubeba mzigo wa kazi za nyumbani na huduma za bila malipo.” 

Wanawake pia wanasalia chini linapokuja siuala la uwakilishi wa maamuzi yanayohusiana na janga la COVID-19 na katika hatua za sera za uchumi kwa ajili ya kukabiliana na janga hilo imeongeza ripoti. 

Pia imeonyesha kuwa “akati janga la COVID-19 limepunguza idadi ya wafanyikazi kwa asilimia 2 kote duniani ikilinganishwa na asilimia 0.2 ya wakati wa mdororo wa kiuchumi wa mwaka 2007-2008, wanawake wengi zaidi ya wanaume walilazimika kuacha kazi kabisa,  na hivyo kupanua pengo la usawa wakijinsia katika ajira na mshahara.” 

Kwa upande wa biashara zinazomilikiwa na wanawake ripoti inasema zimekuwa mbaya zaidi.  

"Janga hili limesukuma karibu wanawake na wasichana milioni 58 katika umaskini uliokithiri, na kusababisha pigo kubwa kwa juhudi za kupunguza umaskini ulimwenguni kote na kuongeza mapengo ya kijinsia katika mapato, utajiri na elimu, na kuzuia maendeleo ya usawa wa kijinsia," amesema Hamid Rashid, Mkuu wa kitengo cha DESA cha ufuatiliaji uchumi duniani na mwandishi mkuu wa ripoti hiyo. 

Ameongeza kuwa "Hatua za kifedha za kusaidia kudhibiti janga hilo na kujikwamua lazima zizingatie athari tofauti za janga hilo kwa makundi tofauti ya watu wakiwemo wanawake, ili kuhakikisha kujikwamua kiuchumi ambako ni jumuishi na kwenye ujasiri.”