Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zote lazima zijitolee kupunguza uzalishaji hewa chafunzi – Antonio Guterres 

Msitu kama huu huko Kalimantan, Indonesia, unaweza kuhifadhi hewa chafuzi na hivyo kusaidia hali ya hewa.
CIFOR/Nanang Sujana
Msitu kama huu huko Kalimantan, Indonesia, unaweza kuhifadhi hewa chafuzi na hivyo kusaidia hali ya hewa.

Nchi zote lazima zijitolee kupunguza uzalishaji hewa chafunzi – Antonio Guterres 

Tabianchi na mazingira

Kutokana na hali mbaya zaidi ya hewa  na majanga ya asili, viwango vya juu vya joto na viwango vya juu vya hewa chafuzi, ubinadamu uko kandoni mwa kuzimu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , António Guterres ameonya hii leo katika mkutano wa tabianchi uliofanyika mjini Petersberg, Ujerumani. 

“Hadi kufikia mwaka jana, wastani wa joto tayari umezidi kiwango cha kabla ya viwanda cha nyuzi joto 1.2 za Selisiasi, ni hatari sana kwani kiwango hiki kinakaribia ukomo ambao jamii ya wanasayansi wameiweka, yaani nyuzi joto 1.5 za Selisiasi.” Amesema Guterres.  

Katibu Mkuu Guterres ameendelea kusema kuwa ikiwa jamii ya kimataifa haiweki juhudi zake zote za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, mwishoni mwa karne hii, wastani wa joto la kila mwaka linaweza kuzidi kiwango cha kabla ya viwanda kwa digrii 2.4 za Selisiasi, na matokeo mabaya yasiyoweza kurekebishwa. 

“Lakini kama tutafanya kazi pamoja, tunaweza kuepuka athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi. Lazima tutumie fursa ambazo zinajitokeza mbele yetu baada ya janga la COVID-19 na kujenga uchumi tayari kulingana na mtindo wa mazingira.” Bwana Guterres amesisitiza na kushauri.  

Aidha Bwana Guterres amebainisha kuwa mataifa mengi tayari yamefanya maendeleo makubwa katika suala la kupunguza athari za ongezeko la joto duniani. Kwa hivyo, mamlaka ya nchi kadhaa, ambazo ni asilimia 73 ya pato la ulimwengu, tayari wameweka ahadi maalum kufikia "uzalishaji wa sifuri" wa hewa chafuzi ifikapo mwaka 2050. 

“Uzalishaji sifuri” inamaanisha kuwa kiwango cha uzalishwaji wa hewa chafuzi hakizidi kiwango kinachoweza kuchukuliwa na bahari pamoja na misitu.  

TAGS: Antonio Guterres, Mabadiliko ya tabianchi, Mkutano wa tabianchi, Petersberg