Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi yako ni kama mama na kujitenga nayo ni mtihani:Mkimbizi Donatien

Wakimbizi wa Burundi wanaorejea wakipimwa COVID-19 katika kituo cha mpito nchini Burundi baada ya kurejea kutoka Rwanda.
© UNHCR/Will Swanson
Wakimbizi wa Burundi wanaorejea wakipimwa COVID-19 katika kituo cha mpito nchini Burundi baada ya kurejea kutoka Rwanda.

Nchi yako ni kama mama na kujitenga nayo ni mtihani:Mkimbizi Donatien

Wahamiaji na Wakimbizi

Kutana na Donatien, mkimbizi wa Burundi aliyeishi Rwanda kwa muda wa miaka 4 na sasa amerejea nyumbani na familia yake kupitia mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wa kurejesha nyumbani wakimbizi kwa hiyari. Donatien anaeleza ni kwa nini yeye mkewe na wanawe wawili wamekata shauri la kurudi nyumbani. 

Mkimbizi Donatien akisema sababu kubwa ya kurundi nyumbani ni kwamba nchi ni kama mzazi na kuishi ukimbizi kunafanya kuhisi kuna kile unachokikosa na ndio maana ameamua na familia yake kurudi nyumbani. 

Alikimbilia Rwanda mwaka 2016 na mkewe na mtoto mmoja wakati machafuko ya kisiadsa yalipowatawanya watu 300,000 , mtoto wa pili amempata ukimbizini Rwanda na sasa yeye na familia yake ya watu wanne wametimiza usemi wa nyumbani ni nyumbani na alipowasili tu anasema,“kitu cha kwanza ni kuzungumza na ndugu,  marafiki na majiraji waliobaki ambao hawakukimbia ili tuweze kujua hatua gani zilizochukuliwa hadi sasa katika jamii yetu, kwani hatujui nini kilitokea baada ya sisi kuondoka. Tunataka kufahamu nini kinachoendelea. Pili tunataka kujua tutaishije maisha ya kila siku kwa sababu sasa tumerejea na tunataka kutumia nguvu zetu kufanyakazi kwa bidi na kupeleka watoto wetu shuleni” 

Donatien na familia yake ni miongoni mwa zaidi ya wakimbizi wa Burundi 145,000  ambao wamerejea nyumbani tangu kuanza kwa zoezi la kuwarejesha kwa hiyari mwaka 2017.

 Na UNHCR inawasaidia wale wanaotaka kurundi nyumbani kama Donatien  kwani inatambua kwamba kuanza upya maisha popote pale na hata ikiwa kwenu wakati umepoteza kila kitu si jambo rahisi