Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jtihada za kulinda kondoo mwekundu ambaye ni tegemeo la jamii ya Maasai nchini Kenya: IFAD

Kondoo wakiwa malishoni.
ILO Photo/John Isaac
Kondoo wakiwa malishoni.

Jtihada za kulinda kondoo mwekundu ambaye ni tegemeo la jamii ya Maasai nchini Kenya: IFAD

Ukuaji wa Kiuchumi

Haki za watu wa asili kusimamia ardhi yao kulingana na mahitaji na maamuzi yao ni suala muhimu katika kulinda tegemeo lao la maisha na pia katika kulinda mifugo asilia na mimea. Ni suala lililo bayana kuwa kuzisaidia jamii za asilia na chakula chao cha kitamaduni inaamnisha ni kulinda bayo anuai duniani.

Jamii ya watu wa Maasai huko Afrika Mashariki wanaishi kwenye bonde la ufa  Kusini mwa Kenya na Kaskazini mwa Tanzania. Tangu jadi wamekuwa ni watu wa kuhamahama na maisha yao ya kila siku yalitemegea ng’ombe, mbuzi na kondoo.

Kuchunga mifugo ni kazi ya wanaume huku kondoo nao wakichungwa na wanawake na watoto. Kuhama kwa mifugo kulitegemea misimu. Kulingana na makubaliano ya umiliki wa ardhi wa tangu jadi katika jamii ya Maasai, hakuna mtu atazuiwa kutumia mali asili kama ardhi na maji.

Miaka ya hivi karibuni jamii ya Maasai imepoteza ardhi kubwa na mali asilia kama ardhi, lishe na chumvi kwa mbuga za wanyama pori.

Hii, pamoja na kuongezeka ukame, hali inayosabaishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, vimechangia kudorora kwa kiwango kikubwa cha tegemeo la maisha kwa jamii ya Maasai.

Kondoo wekundu wa kimaasai, ni aina ya fulani ya kondoo ambayo tangu zamani ilifugwa na jamii ya Maasai na pia  wafugaji wadogo nchini Kenya, Tanzania na Uganda.

Licha ya mazai kuwa madogo wakilinganishwa na wengine, Kondoo hawa hupendwa kwa sababu ya ustaamilifu wao katika mazingira ya ukame na pia dhidi ya athari zingine za kiafya. 

Sababu nyingine ni ladha ya nyama yao ambayo inaelezwa na Wamaasai kama iliyo tamu na hali ya juu ya maziwa yao. Miaka iliposonga Kondoo wekubdu wa kimaasai nusura watoweka na baadaye kondoo aina ya Dorper wakaletwa na Waingereza.

Kikundi cha Slow Food Kenya kilipendekeza aina mpya ya kondoo mwekundu wa kimaasai atunzwe kutokakana na ubora wake na manufaa ambayo yatafuatia ili kuwasaidia jamii wa Maasai kujitoa kwenye hali ngumu waliojipata.

Vikundi viwili vilichaguliwa moja kwenye kaunti ya Nakuru cha Rosarian na kingine katika kaunti ya Narok  cha Olkeri.

Hadi Septemba 2020 mpango huo ulikuwa umepata wanachama 41 , 20 wakiwa  ni vijana wakati walijiunga huku 19 wakiwa ni wanawake. Kushiriki kwa vijana ilikuwa ni lengo la vikundi vyote na vijana wameshirikiana na wazee kufufua tamaduni.

Mpango huo pia uliwapa fursa kubwa wanawake kushiriki kwa kuwa wanawake hutambuliwa kama walio na tajriba katika kutambua wanyama bora.