UNESCO leo imekabidhi tuzo ya Guillermo Cano kwa Maria Ressa

Mwandishi wa habari wa uchunguzi wa Ufilipino leo ametunukiwa tuzo ya heshima kwenye hafla iliyoandaliwa iliyoandaliwa na Serikali ya Namibia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO katika mji mkuu Windhoek, nchini Namibia ambako wataalamu wa vyombo vya habari wanataka hatua za dharura zichukuliwe dhidi ya vitisho na kudhoofishwa kwa uhuru wa habari kote ulimwenguni.
Hafla hiyo iliyofanyika leo Mei 2 na usiku wa kuamkia siku ya uhuru wa vyombo vya Habari duniani, imeandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na serikali ya Namibia ili kutoa Tuzo ya Unesco ya Guillermo Cano kwa mshindi wa mwaka 2021 ambaye ni mwandishi wa habari wa Ufilipino Maria Ressa.
Tayari ameshakamatwa kwa kutumia taaluma ya mwandishi wa Habari za uchunguzi.
Maria Ressa anaendesha wavuti wa habari, ujulikanao kama Rappler, ambao unaripoti visa vya ufisadi na makosa.
Tuzo hiyo ya UNESCO ya dola 25,000 imeanzishwa ili kumuenzi mwandishi wa Habari wa Colombia aliyeuawa