Guterres amelaani vikali shambulio la kujitoa muhanga Afghanistan

1 Mei 2021

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio la kujitoa muhanga lililofanyika jana Ijumaa katika katika eneo la Puli-e-Alam, jimbo Logar nchini Afghanistan.

Kwa mujibu wa duru za habari shambulio hilo limekatili takriban maisha ya watu 27 na kujeruhi wengine wengi ikiwa ni pamoja na kuharibu makazi ya raia, na miundombinu ikiwemo hospitali.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake hii leo mjini New York Marekani, Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha, serikali na watu wa Afghanistan.

Pia amesema anatumai kwamba mfungo wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ambao ni wakati wa kutafakari na kuonesha fadhila utakuwa ni wakati wa kutafakari na kuwakumbuka wale walioathirika na vita vya muda mrefu nchini humo na kuja pamoja katika juhudi mpya za kuelekea amani.

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter