Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takribani watu milioni 3.4 Myanmar wanaweza kukabiliwa na njaa – WFP Myanmar 

Wakimbizi wapokea mgao wao wa chakula.
Picha:: CERF/OCHA
Wakimbizi wapokea mgao wao wa chakula.

Takribani watu milioni 3.4 Myanmar wanaweza kukabiliwa na njaa – WFP Myanmar 

Msaada wa Kibinadamu

Watu wanaokadiriwa kufikia milioni 3.4 nchini Myanmar wanaweza kuingia katika "hatua za wasiwasi za ukosefu wa chakula" kwa miezi sita ijayo na wanahitaji msaada, amesema Marcus Prior ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa WFP nchini humo kupitia mahojiano na UN News. 

Kupitia mahojiano hayo na UN News, Bwana Prior anasema WFP imekuwa na wasiwasi sana kwa muda mrefu juu ya hali ya uhakika wa chakula nchini Myanmar na umaskini uliokuwepo hapo awali uliochangiwa na athari za COVID-19, hasa katika maeneo ya mijini, na pia mzozo wa kisiasa nchini humo. 

Naibu Mkurugenzi huyo wa WFP nchini Myanmar anasema imekuwa miezi "migumu sana" kwa watu wengi klibainisha kuwa kumekuwa na "uhamaji muhimu kuondoka katika eneo la Yangon," na viwanda vingi kwa sasa vimefungwa au vinafanya kazi kwa kiwango cha chini sana na  mfumo wa benki "umepooza nusu, na sio kawaida kuona watu wakipanga foleni katika foleni ndefu ili tu kuchukua pesa." 

Aidha, afisa huyo amesisitiza kuwa hii yote inaongeza katika "hali ya wasiwasi wa kweli na ambao WFP imekadiria kuwa katika miezi sita ijayo takribani watu milioni 3.4 wanaweza kuanguka katika hatua za wasiwasi wa ukosefu wa chakula na wanahitaji msaada kutoka kwetu au kwa wahusika wengine . ” 

Bwana Prior amesema, hata kabla ya COVID-19, WFP ilikuwa na mradi mkubwa sana nchini Myanmar wakileta msaada wa chakula kwa takribani watu milioni moja. Anasema programu hiyo ilikuwa ikifanya kazi kuhakikisha kuwa misaada inatolewa kila siku na ingawa kuna ongezeko la mahitaji mapya, hawawezi kuwaacha watu ambao wako katika mazingira hatarishi na uhitaji lakini moja ya changamoto kubwa ni kiwango cha uhitaji, hasa katika maeneo ya mijini, lakini pia jinsi ya kujipanga katika muktadha kama huo kuhakikisha kuendelea kuwapatia watu wenye uhitaji.  

Akieleza mikakati mipya, Bwana Prior anasema, "tayari tumehamia katika kuweka chakula cha dharura ambacho kitaturuhusu kubadili msaada kutoka pesa taslimu ili kuwa chakula badala yake, ikiwa chakula haitoshi tena , au, ambayo ni moja ya wasiwasi wetu mkubwa, kwamba tatizo la sasa katika sekta ya benki inamaanisha kuwa hatuwezi kupata pesa mkononi ili kufanya miamala kwa watu wanaohitaji. ” 

Kwa mujibu wa Bwana Prior, WFP imeweza kulipia mahitaji ya malipo ya dharura hadi sasa kupitia mchanganyiko wa washirika wapya wa benki na wale waliopo, lakini kama programu inavyoonekana kuongezeka katika maeneo ya mijini na kutoa msaada kote nchini, inapaswa kufanya kazi ndani ya huu muktadha mpya ambapo mifumo ya uwasilishaji misaada ni migumu sana.