Wafanyakazi muhimu wanahitaji ulinzi wakati wa vita dhidi ya COVID-19 yaonya ILO

28 Aprili 2021

Janga la corona au COVID-19 limeanika hatari za mahali pa kazi zinazowakabili wafanyikazi muhimu ambao wanahitaji ulinzi mkubwa zaidi kuweza kufanya kazi zao kwa usalama, limesema leo shirika la kazi laUmoja wa Mataifa (ILO). 

Ripoti mpya ya shirika hilo, iliyotolewa leo kuadhimisha siku ya usalama na afya kazini duniani, imebaini kuwa wafanyikazi wa afya 7,000 wamekufa tangu kuzuka kwa janga la COVID-19, wakati wafanyikazi wengine wa afya na huduma za jamii milioni 136 wako katika hatari ya kuambukizwa COVID-19 kupitia kazi wanazofanya. 

Ripoti hiyo , “Tarajia, andaa na kabiliana na janga: Wekeza sasa katika mnepo wa mifumo ya OSH (Usalama wa Kazini na Afya),” inaangalia jinsi nchi zinavyoweza kupunguza hatari kwa kila mtu mahali pa kazi, endapo kutazuka tena dharura za kiafya hapo baadaye. 

Ripoti hiyo inaangazia pia shinikizo za afya ya akili zinazohusiana na janga hilo: mmoja kati ya wafanyikazi 5 wa huduma ya afya ulimwenguni, ameripoti msongo wa mawazo na dalili za wasiwasi. 

Wanawake katika kiwanda cha nguo Hai Phong nchini Vietnam
© ILO
Wanawake katika kiwanda cha nguo Hai Phong nchini Vietnam

Mifumo thabiti na yenye mnepo 

Ripoti hiyo inabainisha majukumu muhimu yaliyofanywa wakati wa janga la COVID-19 na mwongozo madhubuti wa mahali pa kazi unaoungwa mkono na utekelezaji, na inatoa wito kwa wahudumu hao kuunganishwa na mipango ya dharura ya kitaifa. 

“Hakujawezi kuwa na onyesho la wazi zaidi la umuhimu wa mazingira imara, yenye nguvu,mnepo, usalama kazini na afya. Kujikwamua na kuzuia janga hiuli kutahitaji sera bora za kitaifa, mifumo ya kitaasisi na udhibiti,iwe imejumuishwa vizuri katika mifumo ya kukabiliana na majanga ", amesema Mkurugenzi Mkuu wa ILO Guy Ryder. 

Faida na hasara za kufanyia kazi majumbani 

ILO inasema sio tu sekta za afya na huduma ambazo zimethibitisha kuwa vyanzo vya milipuko ya COVID-19. 

Sehemu nyingi za kazi ambapo wafanyikazi wako katika mazingira ya kujifungia au hutumiamuda mwingi kuwa karibukaribu au pamoja na katika makazi ya pamoja au vyombo vya usafiri wameathirika pia. 

Na wakati kufanyia kazi nyumbani kumekuwa katika kuzuia kuenea kwa virusi, pia kumefifisha mistari wa kati ya kazi na maisha ya faragha, na kuongeza msongo wa mawazo kwa watu. 

Mwanamke akiendesha kigari cha kunyanyua mizigo mizito katika kiwanda nchini Jordan
UNDP/Sumaya Agha
Mwanamke akiendesha kigari cha kunyanyua mizigo mizito katika kiwanda nchini Jordan

Asilimia 65 ya biashara zilizofanyiwa utafiti na ILO na mtandao wa G20 OSH, uliozingatia usalama kazini, wameriripoti kwamba ari ya wafanyikazi imeshuka na imekuwa vigumu kuidumisha wakati wa kufanyia kazi nyumbani. 

Ripoti hiyo imesema “Kwa wafanyabiashara wadogo wadogo imekuwa vigumu kukidhi matakwa ya usalama kazini kwa sababu wengi wamekosa rasilimali ya kukabiliana na vitisho vinavyosababishwa na janga hilo l;a COVID-19.” 

Katika sekta isiyo rasmi, shirika hilo la Umoja wa Mataifa limeonya kuwa wafanyikazi bilioni 1.6 katika sekta hiyo, haswa katika nchi zinazoendelea, wameendelea kufanya kazi licha ya kuzuiliwa, masharti ya kusalia nyumbani na kuhakikisha hakuna mwingiliano wa kijamii. 

Hii imewaweka katika hatari kubwa ya kupata virusi, lakini wengi hawana huduma za msingi za kijamii, kama vile likizo ya ugonjwa au malipo ya ugonjwa. 

Wafanyakazi wa kiwanda  huko Cambodia
ILO/Marcel Crozet
Wafanyakazi wa kiwanda huko Cambodia

Mazungumzo ya kijamii ni muhimu 

Viwango vya kazi vya kimataifa (ILS) vinatoa mwongozo maalum kuhusu jinsi ya kukabiliana na changamoto hizi na kupunguza hatari ya maambukizi ya virusi mahali pa kazi, imesema ripoti 

Vinatoa zana za kutekeleza hatua za kwanza za usalama na kuhakikisha kuwa wafanyikazi, waajiri na Serikali, wanaweza kudumisha ajira zenye hadhi, huku wakirekebisha matokeo ya kijamii na kiuchumi ya athari za janga hilo. 

Ripoti inahitimisha kuwa, ILS pia inahimiza mazungumzo ya kijamii kama njia bora ya kuhakikisha kuwa taratibu na itifaki zinatekelezwa na kukubalika, ripoti inahitimisha. 

 

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter